-
Umoja wa Mataifa wataka wakaguzi wa kimataifa waruhusiwe kufika maeneo yote ya Gaza
Sep 16, 2026 02:55Umoja wa Mataifa umeashiria kugunduliwa mamia ya miili chini ya vifusi katika Ukanda wa Gaza na kutoa wito wakaguzi wa kimataifa waruhusiwe kuingia na kufika katika maeneo yote ya ukanda huo ili kukusanya ushahidi na kuchunguza uwezekano wa kutendeka uhalifu wa kivita.
-
Askari wa Israel asema waliambiwa: 'Mnao watu milioni mbili wa kuwalenga shabaha Ghaza'
Sep 13, 2026 07:05Askari wa akiba wa jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel amesema, maafisa wa jeshi hilo wanaichukulia idadi yote ya Wapalestina milioni mbili wa Ukanda wa Ghaza kama walengwa halali wa kuuawa, na amesimulia mauaji mengi yaliyofanywa na askari wa kizayuni na jinsi utekelezaji wa kanuani za vita ulivyoporomoka wakati wa mauaji ya kimbari ya Wapalestina wa eneo hilo.
-
Ripoti: Watu 8,000 wamekatwa viungo tangu kuanza kwa vita dhidi ya Gaza
Sep 10, 2026 03:19Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Quds (Qudsna), vyanzo vya Palestina vimeripoti kwamba tangu kuanza vita dhidi ya Gaza, visa 8,000 vya kukatwa viungo vya mwili vimeripotiwa. Aidha, katika hali ya sasa, watu 10,000 wenye ulemavu wa viungo wanahitaji huduma za urekebishaji na tiba ya viungo kwa dharura.
-
Nchi nane za Kiarabu na Kiislamu: Gaza ni eneo lisiloweza kutenganishwa na Palestina
Sep 07, 2026 03:05Nchi nane za Kiarabu na Kiislamu ambazo ni Saudi Arabia, Jordan, Umoja wa Falme za Kiarabu, Indonesia, Pakistan, Uturuki, Qatar na Misri, zimetangaza kuwa, Ukanda wa Gaza ni sehemu isiyotenganishwa ya ardhi ya Palestina.
-
Umoja wa Mataifa: Hakuna sehemu salama katika Ukanda wa Gaza
Sep 07, 2026 02:56Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, hakuna sehemu salama katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.
-
Mazishi ya Wapalestina 100 waliouliwa shahidi yafanyika Gaza; watoto 70 ni miongoni mwa mashahidi hao
Sep 06, 2026 11:32Mazishi ya Wapalestina 100 waliouliwa shahidi yafanyika Gaza; watoto 70 ni miongoni mwa mashahidi hao
-
UN: Hali ya kibinadamu Gaza na Ukingo wa Magharibi yazidi kuzorota
Sep 02, 2026 02:43Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na la Afya Duniani (WHO) yameonya kuhusu kuzorota kwa hali ya kibinadamu katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu na Israel.
-
Afrika Kusini yawasilisha kesi ICJ dhidi ya Israel kwa kukataa kutekeleza maamuzi yake kuhusu Gaza
Aug 30, 2026 03:42Afrika Kusini imewasilisha hati mpya ya ushahidi kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), ikiishutumu Israel kwa kukataa kufuata maagizo matatu ya kisheria kuhusu Ukanda wa Gaza, na kuonya kwamba kuendelea ukiukwaji wa sheria za kimataifa kunaweza kudhoofisha himaya inayotolewa na mahakama hiyo na uhalali wake.
-
Baada ya miaka 25, Misri yamtambulisha tena mtoto Muhammad al-Durra kwenye mtaala wa somo la historia
Aug 26, 2026 11:13Miaka 25 baada ya tukio lililoishtua na kuitikisa dunia, picha ya mtoto wa miaka 12 wa Kipalestina Muhammad al-Durra aliyeuliwa kinyama na hadharani na jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel imehama kutoka kwenye skrini za televisheni hadi kwenye kurasa za kitabu cha kiada cha Misri, katika somo linaloangazia Intifadha ya Pili ya Wapalestina ya mwaka 2000.
-
Umoja wa Mataifa: Hali ya kibinadamu Ukanda wa Gaza ni mbaya kutokana na kuongezeka wimbi la njaa
Aug 22, 2026 02:53Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu kuzidi kuwa mbaya hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza kutokana na kuendelea mashambulizi ya utawala wa Israel pamoja na kushadidishwa mzingiro dhidi ya eneo hilo.