-
HAMAS yakaribisha mpango wa Waarabu wa kuijenga upya Gaza
Mar 06, 2025 02:26Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imekaribisha mpango wa kuikarabati na kuijenga upya Gaza, uliopitishwa katika mkutano wa dharura wa viongozi wa nchi za Kiarabu mjini Cairo, Misri. Mpango huo pia unakusudia kuzuia kuondolewa Wapalestinakatika eneo hilo lililo chini ya mzingiro.
-
Misri yapinga pendekezo la Israel la kutaka Gaza isimamiwe na Cairo
Feb 27, 2025 11:01Misri imepinga pendekezo lililotolewa na kiongozi wa upinzani wa Israel, Yair Lapid kwamba Cairo, badala ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas, iendeshe na kuusimamia kwa muda Ukanda wa Gaza; na kusisitiza kuwa mipango ya aina hiyo "haikubaliki."
-
Kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina; Jinai mpya dhidi ya Wapalestina
Feb 20, 2025 08:10Leo tutaangazia jinai mpya ya Wazayuni na washirika wao ya kutaka kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina katika makazi na nchi yao.....
-
Israel kuunda 'wakala wa kuwafukuza' Wapalestina Gaza
Feb 18, 2025 07:30Wizara ya Vita ya Israel imesema ipo mbioni kuunda chombo mahsusi cha utawala huo wa Kizayuni cha kushughulikia eti "kuondoka kwa khiari" raia wa Palestina kutoka Gaza.
-
Mahathir azikosoa EU, US kwa mauaji ya kimbari Gaza, asema 'Ustaarabu umefeli'
Feb 15, 2025 07:16Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia amekosoa vikali uungaji mkono wa Marekani na Umoja wa Ulaya kwa Israel akisisitiza kuwa, kuunga mkono kwa hali na mali mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza ni jambo la 'kuchukiza na kukirihisha.'
-
Kundi la Waarabu UN lapinga kufurushwa Wapalestina Gaza
Feb 15, 2025 07:14Kundi la Waarabu katika Umoja wa Mataifa, pamoja na kundi la mabalozi wa Umoja wa Mataifa, wamepinga vikali mipango yoyote ya "kuwaondoa kwa nguvu" Wapalestina huko Gaza, na kusisitiza kuwa hatua hiyo ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.
-
Jihadul Islami: Hatutaruhusu kufukuzwa Wapalestina Gaza
Feb 14, 2025 12:09Mwakilishi wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina mjini Tehran amesema Wapalestina kamwe hawatakubali kutekelezwa mpango wa Marekani wa kuwaondoa kwa nguvu wakazi wa Gaza.
-
Mwanasheria Mmarekani: Israel imeua Wapalestina 360,000 Gaza
Feb 13, 2025 02:51Mwanasheria mashuhuri wa Marekani na mwanaharakati wa haki za watu asilia anakadiria kuwa jeshi la Israel limewaua takriban watu 360,000 katika vita vyake vya mauaji ya kimbari vilivyodumu kwa muda wa miezi 15 katika Ukanda wa Gaza, akisema kwamba idadi ya vifo vya kweli katika eneo lililozingirwa ni kubwa zaidi kuliko takwimu iliyoripotiwa na vyombo vya habari.
-
Pezeshkian: Mataifa ya Kiislamu yaungane kuijenga upya Gaza
Feb 09, 2025 07:14Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian ametoa mwito kwa nchi za Kiislamu kuungana na kushirikiana ili kulijenga upya eneo la Ukanda la Gaza ambalo limeharibiwa kikamilifu na mabomu ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Iran yataka OIC iitishe mkutano wa dharura kuijadili Gaza
Feb 09, 2025 07:11Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amekosoa vikali mpango wa pamoja wa Marekani na Israel wa kuwahamisha raia wa Gaza, na maangamizi ya kizazi katika eneo hilo lililozingirwa.