-
UNICEF: Watoto laki tano wanakabiliwa na hatari ya kifo Somalia kutokana na uhaba wa chakula
Sep 17, 2022 07:54Msemaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) amesema katika taarifa kwamba, watoto nusu milioni nchini Somalia wanakabiliwa na hatari ya kifo kutokana na uhaba wa chakula na utapiamlo.
-
Indhari ya UNICEF: Idadi ya watoto wanaokosa masomo kwa sababu ya majanga imeongezeka sana
Jun 22, 2022 07:56Mfuko wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa kuhusu elimu kwenye maeneo yenye dharura na majanga, ECW umetoa ripoti ya kutisha ikidokeza kuwa idadi ya watoto wenye umri wa kwenda shule, ambao wameathirika na majanga na hivyo kuhitaji msaada wa kielimu imeongezeka kutoka milioni 75 mwaka 2016 hadi milioni 222 hii leo.
-
UNICEF: Kwa akali watoto 17 wameuawa nchini Yemen tangu kuanza mwezi huu wa Januari
Jan 23, 2022 12:20Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, kwa akali watoto 17 wameuawa nchini Yemen tangu kuanza mwezi huu wa Januari kufuatia mashambulio ya anga ya muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia.
-
UNICEF: Pande zinazozozana Tigray Ethiopia zimefanya ukandamizaji dhidi ya watoto
Jan 10, 2022 13:46Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umezituhumu pande zinazopigana katika jimbo la Tigray la kaskazini mwa Ethiopia kwamba, zimefanya ukandamizaji mkubwa dhidi ya watoto.
-
UNICEF: Ukiukaji wa haki za watoto umekithiri duniani
Jan 01, 2022 03:33Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limesema mwaka uliomalizika wa 2021 umekuwa wa machungu na ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto katika mizozo ya muda mrefu na ile mipya iliyojitokeza katika nchi mbalimbali duniani.
-
UNICEF yaonya kuhusu hali mbaya ya watoto milioni moja nchini Afghanistan
Oct 31, 2021 02:20Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) umetahadharisha kuwa, watoto milioni moja wa Afghanistan wako katika hali mbaya na hatari ya kupoteza maisha kutokana na lishe duni.
-
Watoto wa Kiafghani zaidi ya milioni nne hawaendi shule
Sep 19, 2021 06:47Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umeripoti kuwa watoto wa Kiafghani zaidi ya milioni nne hawajajiandikisha kuanza shule mwaka huu nchini humo.
-
UNICEF: Ndani ya kila dakika 10, mtoto anaaga dunia Yemen
Aug 24, 2021 08:01Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) ametahadharisha kuhusu hali ya kibinadamu inayozidi kuwa mbaya nchini Yemen kutokana na vita vinavyoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo masikini ya Kiarabu na kusema kuwa, mtoto mmoja wa Yemen hupoteza maisha kila baada ya dakika 10.
-
UNICEF: Maisha ya watoto bilioni moja yako hatarini kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi
Aug 21, 2021 12:55Ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF inaonyesha kuwa, vijana na watoto bilioni moja duniani hususan wanaoishi katika nchi za Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Nigeria, Guinea, na Guinea-Bissau wanakabiliwa na hatari zaidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi, yakitishia afya zao, elimu, na ulinzi, na kuwaweka kwenye hatari ya magonjwa.
-
Njama za UNICEF za "kurubuni" watoto wa Yemen zagunduliwa al Hudaydah
May 03, 2021 07:50Maafisa wa Yemen katika mkoa wa al Hudaydah wamegundua shehena iliyotumwa na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) kama zawadi kwa waototo wa Yemen ambayo ina mifuko ya shule na ramani zinazoutambua rasmi utawala haramu wa Israel badala ya Palestina.