-
Kwa wiki ya 85 mtawalia utawala wa Bahrain wazuia kusaliwa Sala ya Ijumaa eneo la Ad Diraz
Mar 03, 2018 04:39Askari wa utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain jana walizuia kwa wiki ya 85 mtawalia kusaliwa Sala kubwa zaidi ya Ijumaa ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika eneo la Ad Diraz.
-
Nabeel Rajab ahukumiwa kifungo cha miaka 5 jela nchini Bahrain
Feb 22, 2018 04:29Nabeel Rajab, mwanaharakati mashuhuri wa masuala ya haki za binadamu nchini Bahrain amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kile kilichoelezwa kwamba, ni kupatikana na hatia ya uchochezi na jumbe za kukosoa utawala wa nchi hiyo.
-
Wanamapinduzi wa Bahrain wasisitiza kuhitimishwa enzi za utawala uliooza wa Aal Khalifa
Feb 15, 2018 08:21Kiongozi mmoja wa harakati ya Muungano wa Vijana wa Mapinduzi ya Februari 14 ya Bahrain amesema: Wanamapinduzi watapinga mpango wowote ule utakaolenga kuubakisha madarakani utawala wa Aal Khalifa.
-
Wimbi la pili la maandamano ya wananchi nchini Bahrain laanza kwa mnasaba wa Februari 14
Feb 14, 2018 16:49Wimbi la pili la maandamano na harakati ya malalamiko ya wananchi nchini Bahrain kwa mnasaba wa mwaka wa saba wa mapinduzi ya tarehe 14 Februari, limeanza jioni ya leo Jumatano katika maeneo tofauti ya nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Utawala wa Bahrain wawahukumu makumi ya raia adhabu ya kifo, kifungo cha maisha jela na kuwavua uraia
Jan 31, 2018 15:27Mahakama ya Jinai ya Bahrain leo imeendeleza sera kandamizi za utawala wa kiimla wa Aal Khalifa kwa kuwahukumu adhabu ya kifo, kifungo cha maisha jela na kuwavua uraia makumi ya raia wa nchi hiyo.
-
Mkuu wa Kituo cha Haki za Binadamu Bahrain: Hukumu dhidi ya wapinzani ni ulipizaji kisasi
Jan 25, 2018 13:36Mkuu wa Kituo cha Haki za Binadamu cha nchini Bahrain amesema kuwa hukumu zilizotolewa na mahakama dhidi ya wapinzani nchini humo ni za kisiasa na ulipizaji kisasi.
-
Utawala wa Bahrain waendelea kuwakandamiza wapinzani
Jan 23, 2018 14:12Utawala wa kiimla wa Bahrain unaendelea kutumia wanajeshi wake kuwakandamiza wananchi wanaoandamana kwa amani wakitaka utawala wa demokrasia katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.
-
Mwakilishi wa Baraza la Maulama Bahrain: Waislamu wanahitajia umoja ili kuzifukuza Marekani na Israel katika eneo
Dec 06, 2017 15:15Sheikh Abdullah al Daqaq mwakilishi wa Baraza la Maulama la Bahrain na ambaye pia ni mwakilishi wa Ayatullah Sheikh Issa Qassim wa nchi hiyo amesisitiza hapa Tehran juu ya umuhimu wa kuwa na umoja katika hali ya hivi sasa katika ulimwengu wa Kiislamu na kueleza kuwa Waislamu wanahitajia umoja ili kuzifukuza Marekani na Israel katika eneo.
-
Utawala wa Bahrain umekusudia kumuua kwa njia isiyo ya moja kwa moja Ayatullah Sheikh Isa Qassim
Dec 03, 2017 07:16Mjumbe mwandamizi wa Umoja wa Maulamaa wanaounga mkono Muqawama amesema hatua za utawala wa Bahrain dhidi ya kiongozi wa kidini wa nchi hiyo Ayatullah Sheikh Isa Qassim ni sawa na kumuua mwanazuoni huyo wa Kiislamu kwa njia isiyo ya moja kwa moja.
-
Wafungwa wa kisiasa Bahrain wazuiliwa kuwa na mawasiliano yoyote na nje ya jela
Nov 19, 2017 07:55Duru zenye uhusiano na familia ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kitaifa ya al-Wifaq nchini Bahrain, zimeeleza kuwa utawala wa Aal-Khalifa umemwekea vizuizi vikubwa Sheikkh Ali Salman na shakhsia wengine mashuhuri wanaoshikiliwa katika jela za nchi hiyo.