-
Wazayuni wauvamia tena Msikiti wa Al Aqsa kwa siku ya nne mfululizo
Oct 03, 2023 04:23Kundi kubwa la walowezi wa Kizayuni leo wameuvamia tena kwa siku ya nne mtawalia Msikiti wa Al-Aqsa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu huku wakilindwa na kusindikizwa na askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
-
Ukumbusho na indhari ya Iran kwa UN kuhusu utambulisho na matokeo ya vitisho vya utawala wa Kizayuni
Sep 29, 2023 00:29Amir Saeid Iravani Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amewaandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la UN na Rais wa Baraza la Usalama la umoja huo kuhusu matamshi ya vitisho ya karibuni ya waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran.
-
Palestina: Tunapigana vita na utawala wa Kizayuni wa Israel katika medani nne
Sep 28, 2023 11:33Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema, Mpango wa Amani wa Waarabu ni msingi wa kukubalika na pande zote kuhusiana na kadhia ya Palestina na akasisitiza kuwa, wananchi wa Palestina wanapigana vita na utawala wa Kizayuni wa Israel katika medani nne.
-
Hamas: Kuwafungulia njia Wazayuni huko Hijaz kuna maana ya kukubali kukaliwa kwa mabavu Palestina
Sep 27, 2023 23:31Kiongozi mmoja wa harakati ya Hamas amekosoa hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kuranzisha uhusiano na mapatano na utawala wa Kizayuni wa Israel na kusisitiza kuwa, kuwafungulia njia wavamizi wa Israel kwa ajili ya kuingia katika ardhi ya Hijaz (Saudia) kuna maana ya kukubali kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.
-
Jerusalem Post: Satalaiti ya "Nour 3" inaimarisha uwezo wa anga wa Iran
Sep 27, 2023 23:30Gazeti la Jerusalem Post la Israel limeandika kuwa, kurushwa angani Satalaiti Nour 3 ni sehemu ya mafanikio mapya ya kiteknolojia ambayo Iran inatumia kudhihirisha uwezo wake.
-
Hamas: Congo DR inapaswa kuangalia upya uamuzi wa kuhamishia ubalozi wake Quds
Sep 24, 2023 02:28Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani uamuzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv hadi Quds inayokaliwa kwa mabavu (Jerusalem) na kutaka kuangaliwa upya uamuzi huo.
-
Walowezi wa Kizayuni wavamia tena msikiti wa al-Aqswa
Sep 18, 2023 23:01Sambamba na maadhimisho ya sikukuu za Kiyahudi, makumi ya walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya kufurutu ada wameuvamia msikiti mtakatifu wa al-Aqswa na kufanya vitendo vya kichochezi.
-
Iran: Mauaji ya kinyama ya Sabra na Shatila ni doa la aibu kwa waungaji mkono wa utawala wa Kizayuni
Sep 16, 2023 08:46Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mauaji ya Wapalestina wa Sabra na Shatila yaliyofanywa na askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameandika ujumbe usemao: Sabra na Shatila daima litabaki kuwa doa la aibu kwenye vipaji vya waungaji mkono wa utawala wa Israel na watetezi wa kizandiki wa haki za binadamu hususan Marekani na Uingereza.
-
Msikiti wa al-Aqswa waendelea kuvamiwa na walowezi wa Kizayuni
Sep 13, 2023 07:42Walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya kufurutu ada wamevamia msikiti wa al-Aqswa huko Palestina na kuuvunjia heshima.
-
Zaidi ya asilimia 70 ya Wazayuni wanampinga Netanyahu
Sep 10, 2023 03:59Matokeo ya uchunguzi wa hivi karibuni zaidi uliofanywa na vyombo vya habari vya Kizayuni yanaonyesha kuwa, asilimia 75 ya Wazayuni hawaridhishwi na utendaji kazi wa Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni na baraza lake la mawaziri.