Zaidi ya asilimia 70 ya Wazayuni wanampinga Netanyahu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i102058-zaidi_ya_asilimia_70_ya_wazayuni_wanampinga_netanyahu
Matokeo ya uchunguzi wa hivi karibuni zaidi uliofanywa na vyombo vya habari vya Kizayuni yanaonyesha kuwa, asilimia 75 ya Wazayuni hawaridhishwi na utendaji kazi wa Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni na baraza lake la mawaziri.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 10, 2023 03:59 UTC
  • Zaidi ya asilimia 70 ya Wazayuni wanampinga Netanyahu

Matokeo ya uchunguzi wa hivi karibuni zaidi uliofanywa na vyombo vya habari vya Kizayuni yanaonyesha kuwa, asilimia 75 ya Wazayuni hawaridhishwi na utendaji kazi wa Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni na baraza lake la mawaziri.

Uchunguuzi huo wa maoni unaonyesha kuwa, asilimia 55 ya washiriki hawaridhiki na waziri yeyote wa baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Netanyahu.

Imeelezwa katika ripoti hii, kwa upande mwingine, asilimia 35 ya washiriki wa utafiti huu pia wanaamini kwamba Itamar Ben Guer, Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni, amefanya mambo ya kukatisha tamaa zaidi kuliko mawaziri wengine wa baraza la mawaziri.

Wakati huo huo, wapinzani wa mpango wa Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel wa kufanyia mageuzi mfumo wa mahakama wameendelea kuandamana na kuzidi kutishia uhai wa serikali ya Netanyahu na washirika wake.

 

Maelfu ya walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakiandamana kwa zaidi ya miezi miwili sasa kupinga mpango huo wa mageuzi ya mahakama unaoshinikizwa na Netanyahu. Wazayuni wanapinga pia serikali ya Netanyahu yenye mawaziri wenye misimamo ya kufurutu ada.

Uamuzi wa baraza la mawaziri la Netanyahu wa kubadilisha mfumo wa mahakama wa utawala wa Kizayuni umeibua mivutano ya kisiasa na hitilafu kali kati ya muungano unaotawala na mrengo wa upinzani, na hivyo kuongeza maonyo kuhusu uwezekano wa kuibuka vita vya wenyewe kwa wenyewe miongoni mwa Wazayuni wanaokalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina