-
Meli ya nne ya mafuta ya Iran yaingia katika maji ya Venezuela
May 28, 2020 05:37Meli ya nne ya mafuta ya Iran imewasili katika Eneo Mahsusi la Kiuchumi Baharini (EEZ) kwa lengo la kufikisha mafuta ya petroli na dizeli katika nchi hiyo inayokabiliwa na vikwazo vya Marekani.
-
Rais Rouhani aihutubu Marekani: Biashara yetu na Venezuela haiwahusu
May 27, 2020 21:53Rais Hassan Rouhani wa Iran ameikosoa vikali Marekani kwa kujaribu kuingilia miamala ya kibiashara baina ya Jamhuri ya Kiislamu na nchi nyingine huru duniani.
-
Waziri wa Mafuta wa Venezuela: Meli za mafuta za Iran ni nembo ya udugu na mshikamano
May 26, 2020 02:54Waziri wa Mafuta wa Venezuela ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kutuma mafuta nchini humo na kusema kuwa meli za mafuta za Iran zilizotumwa nchini Venezuela licha ya vitisho na vikwazo vya Marekani, ni nembo ya udugu na mshikamano baina ya Tehran na Caracas.
-
Sisitizo la Venezeula kuhusu kutokuwa na maana vitisho vya Marekani dhidi ya meli za mafuta za Iran
May 25, 2020 06:01Wakati wa utawla wa rais Donald Trump wa Marekani, sera za mashinikizo ya pande zote dhidiya Venezeula zimeongezeka kwa kuwekewe vikwazo vingi nchi hiyo lengo likiwa ni kuipindua serikali ya Rais Nicolas Maduro na kumleta madarakani kinara wa wapinzani Juan Guaid ambaye ni kibaraka wa Washington.
-
Venezuela yaishukuru Iran kwa kuifikishia mafuta na kuvunja vikwazo vya Marekani
May 24, 2020 23:28Mwakilishi wa Venezuela katika Umoja wa Mataifa ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baada ya meli ya kwanza ya mafuta ya Iran kuingia katika maji ya nchi hiyo na kusema kuwa, hii ni hatua muhimu sana katika kupambana na ubeberu wa Marekani na kupigania haki ya kujitawala, uhuru na amani.
-
Maneva ya mizinga ya jeshi la Venezuela katika kukaribia kuwasili meli za mafuta za Iran katika maji ya Caribbean
May 24, 2020 04:25Katika hali ambayo ikulu ya Marekani ya White House inatekeleza vikwazo vikali zaidi vilivyo kinyume na ubinaadamu dhidi ya raia na serikali ya Venezuela kwa lengo la kuiondoa madarakani serikali halali ya Rais Nicolás Maduro, kuongezeka ushirikiano wa kibiashara kati ya Tehran na Caracas na kutumwa meli za mafuta zilizosheheni nishati hiyo muhimu huko Venezuela, kumewaongezea hasira viongozi wa Marekani.
-
Venezuela yaionya tena Marekani kuhusu vitisho dhidi ya meli za mafuta za Iran
May 23, 2020 22:14Mwakilishi wa Venezuela katika Umoja wa Mataifa sambamba na kuionya Marekani, amesisitiza kuwa vitisho vya kijeshi vinavyotolewa na Washington dhidi ya meli za mafuta za Iran, havikubaliki.
-
Russia na Venezuela zakosoa hatua zisizo za kisheria za Marekani
May 22, 2020 02:00Tangu Rais Donald Trump mwenye kashfa nyingi wa Marekani aingie ikulu ya White House ameshadidisha siasa za uhasama dhidi ya Venezuela ambapo pia amefanya njama nyingi za kuiondoa madarakani serikali halali ya Rais Nicolás Maduro wa nchi hiyo sambamba na kuiwekea vikwazo vikali.
-
Kukiri John Bolton juu ya kugonga mwamba siasa za Marekani dhidi ya Venezuela
May 19, 2020 05:54Vikwazo na mashinikizo ya Marekani dhidi ya Venezuela yanaendelea katika hali ambayo, kivitendo nchi hiyo ya Amerika ya Latini ikipata msaada wa mataifa kama Iran, China na Russia imefanikiwa kuyapatia ufumbuzi akthari ya matatizo yaliyosababishwa na vikwazo vya Washington.
-
Rais wa Venezuela: Njama iliyofeli ya mapinduzi ilipangwa ndani ya Ikulu ya White House
May 15, 2020 02:54Rais Nicolás Maduro wa Venezuela amesema, njama ya jaribio la mapinduzi lililofeli dhidi ya serikali ya nchi hiyo ilipangwa na kuandaliwa ndani ya Ikulu ya rais wa Marekani ya White House.