Pars Today
Wakuu wa Kanisa Katoliki katika mji wa Quds tukufu unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel wamemuandikia barua Waziri Mkuu wa utawala huo ghasibu wakikosoa misimamo yake ya kibaguzi.
Jumuiya ya Waislamu wa Marekani imefanikiwa kukusanya mchango wa makumi ya maelfu ya dola katika juhudi zao za kuwasaidia wahanga wa shambulizi la kigaidi lililotokea katika hekalu la Kiyahudi la mjini Pittsburgh na kuua watu 11 na kujeruhi wengine sita.
Baraza la Kiislamu-Kikristo la Kuunga Mkono Quds Tukufu (Jerusalem) limetangaza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unatekeleza njama za kuwatimua Wakristo kutoka Quds ili kubadilisha muundo wa kijamii wa mji huo uwe ni aghalabu wa Mayahudi.
Askofu wa Kanisa la Armenia mjini Tehran amesisitiza kuwa, Wakristo hawatambui serikali inayojiita Israel.
Mchungaji wa Kanisa la Anglikana la nchini Uingereza amesema kuwa, Wakristo wa nchi za Magharibi wanafanya kosa kubwa kuamini kuwa kuuunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel ni jukumu lao la kidini.
Zimebakia siku chache tu hadi siku ya Arubaini ya Imam Hussein (as) na barabara zote za kuelekea katika mji wa Karbala nchini Iraq zimefurika watu kama mto wa maji unaoelekea katika mji mtakatifu wa Karbala.
Kiongozi wa Kikristo wa kanisa la Orthodox huko Palestina Atallah Hanna, ameomba msaada wa haraka kutoka kwa Wakristo na taasisi za kutetea haki za binaadamu duniani, kuzuia uvamizi wa Wazayuni wa Israel huko Quds.
Haafidh wa Qur'ani tukufu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema Wakongomani wana hamu na shauku kubwa ya kujifunza Uislamu kiasi kwamba Wakristo wa nchi hiyo wanawapeleka watoto wao madrasa ili wakasomeshwe Qur'ani.
Mufti wa Misri amesema kuwa asilimia 90 ya hukumu na fatwa za watu wanaofurutu ada zinawachochea watu kwenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kuzusha mifarakano baina ya Waislamu na Wakristo.
Makumi ya familia za Wakristo zimelazimika kukimbia makazi yao katika mkoa wa Sinai Kaskazini nchini Misri kutokana na mashambulizi ya watu wenye silaha.