Mchungaji Sizer: Wakristo wanafanya kosa kubwa kuiunga mkono Israel
(last modified Sat, 18 Nov 2017 15:20:16 GMT )
Nov 18, 2017 15:20 UTC
  • Mchungaji Sizer: Wakristo wanafanya kosa kubwa kuiunga mkono Israel

Mchungaji wa Kanisa la Anglikana la nchini Uingereza amesema kuwa, Wakristo wa nchi za Magharibi wanafanya kosa kubwa kuamini kuwa kuuunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel ni jukumu lao la kidini.

Shirika la habari la IRIB limemnukuu Mchungaji Stephen Robert Sizer akisema hayo katika kikao cha "Karne Moja ya Mgogoro" kilichofanyika kwa mnasaba wa kukumbuka siku lilipotolewa tangazo la Balfour mjini London Uingereza na kusema kuwa, tangazo hilo limepelekea kukanyagwa haki za Wapalestina na kusababisha zaidi ya Wapalestina milioni 7 kuwa wakimbizi.

Mchungaji Sizer ameongeza kuwa, vita vya Israel dhidi ya Wapalestina vinaweza kugeuka kuwa vita vikali sana vya kidini kwani vinaweza kuwatumbukiza kwenye vita visivyo na mwisho; Wakristo, Mayahudi, Waislamu na Waduruzi.

Kanisa la Miracle lilichomwa moto na Wazayuni huko Palestina. Utawala wa Kizayuni wa Israel hauheshimu mafundisho yoyote ya dini yanayopinga jinai zake

 

Mchungaji huyo wa Kanisa la Anglikana la nchini Uingereza amegusia nafasi muhimu ya nchi hiyo katika kuunda utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema kuwa, ushahidi uliopo unaonesha kwamba, muswada wa azimio la Balfour uliandikwa mara tatu na Wazayuni ndipo baadaye likapatikana azimio la mwisho.

Azimio la Balfour lilitolewa tarehe pili Novemba 1917 na Arthur James Balfour, waziri wa mambo ya nje wa wakati huo wa Uingereza akimpelekea Walter Rothchild, mwanasiasa Mzayuni aliyekuwa mbunge katika bunge la Uingereza wakati huo na azimio hilo ndio msingi wa kuundwa utawala ghasibu wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina.

Tags