Askofu Mkuu wa Ghana: Taswira ya Iran inaheshimiwa miongoni mwa Wakristo
(last modified Sun, 05 Jan 2025 07:53:34 GMT )
Jan 05, 2025 07:53 UTC
  • Askofu John Bonaventure Kwofie
    Askofu John Bonaventure Kwofie

John Bonaventure Kwofie, Askofu Mkuu wa Ghana na Kiongozi wa Wakatoliki wa nchi hiyo ameeleza kuwa taswira ya Iran inaheshimiika na kuaminika miongoni mwa waumini wa Kikristo.

Amir Heshmati, Mwambata wa Masuala ya Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Ghana, na Askofu Mkuu John Bonaventure Kofi, Kiongozi wa Wakatoliki wa nchi hiyo wamekutana na kuzungumza katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Miladia. 

Mwambata wa Utamaduni wa Iran mjini Accra ameshukuru misimamo ya kiongozi wa Wakatoliki wa Ghana kuhusu suala la taasisi ya familia na haja ya kuishi pamoja kwa amani wafuasi wa dini na makabila mbalimbali nchini humo na akasema, kufanyika mazungumzo baina ya dini mbalimbali ni fursa ya kipekee ya kufungua kurasa mpya ili kuzipatia suluhisho mujarabu daghadagha na changamoto mbalimbali za dunia ya leo. Amir Heshmati amemwalika pia Askofu Mkuu wa Ghana kutembelea Iran. 

Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Ghana amesema Iran inaheshimika na kuaminika miongoni mwa Wakristo na kwamba yupo tayari kufanya ziara hapa nchini katika siku chache zijazo ili kutembelea maeneo ya kitamaduni na kidini ya Iran  na kuzungumza na wanafikra wa kidini.