-
Polisi Kenya yawaonya wanasiasa, yataka notisi za mikutano, maandamano zitolewe siku 3 kabla
Sep 06, 2026 02:59Jeshi la Polisi la Kenya (NPS) limewaonya viongozi wa kisiasa na wafuasi wao kwamba litatekeleza kikamilifu Sheria ya Utulivu wa Umma wakati nchi hiyo inaingia katika kipindi cha kampeni za uchaguzi.
-
Niger: Jaribio la uasi wa jeshi lilichochewa na mtandao mpana ukiongozwa na Ufaransa
Sep 06, 2026 02:57Serikali ya Niger imeishutumu Ufaransa kwa kuchochea shambulio dhidi ya kituo muhimu cha jeshi la anga lililofanywa na wanajeshi walioasi wiki iliyopita.
-
DRC yazindua mpango mpya wa mapambano dhidi ya Ebola, yatafuta msaada wa dola bilioni 1.3
Sep 05, 2026 12:05Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na washirika wake wamezindua siku ya Ijumaa mpango mpya wa sekta mbalimbali wa siku 180 unaolenga kuimarisha juhudi dhidi ya mlipuko wa sasa wa Ebola, huku mahitaji ya fedha yakikadiriwa kufikia dola bilioni 1.3 za Kimarekani.
-
UN yaidhinisha ombi la Afrika la kuichora tena ramani ya dunia, Marekani yapinga
Sep 05, 2026 11:28Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Ijumaa ya Septemba 04 limeidhinisha azimio la kura 164 za ndio na 1 ya hapana, linalolenga kurekebisha namna mabara yanavyoonekana kwenye ramani. Marekani ndiyo nchi pekee iliyopiga kura kulipinga azimio hilo.
-
Gesi ya sumu yaua watu 43 wakati wa wizi wa mafuta nchini Nigeria
Sep 05, 2026 02:57Takriban watu 43 wamefariki dunia baada ya kuvuta gesi yenye sumu wakati wa operesheni haramu ya kuvuta mafuta kwenye bomba katika Jimbo la Rivers, kusini mwa Nigeria.
-
Africa CDC: Ni mapema mno kutangaza mripuko wa Ebola umedhibitiwa DRC
Sep 04, 2026 10:38Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (Africa CDC) vimetangaza kuwa bado ni mapema mno kusema kwamba mripuko wa Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umedhibitiwa, licha ya kuweko dalili za kupungua sana ugonjwa huo katika wiki za hivi karibuni.
-
WFP yalaani mashambulizi dhidi ya malori ya misaada kusini mwa Sudan
Sep 04, 2026 03:18Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limetangaza kwamba malori yake mawili yalishambuliwa kutokea angani siku ya Jumapili nje ya eneo la Dilling la Jimbo la Kordofan Kusini, huko kusini mwa Sudan, wakati yalipokuwa njiani kupeleka chakula cha msaada kwa wakimbizi waliokwama kwenye eneo la Kadugli.
-
Jeshi la Niger lakamata silaha baada ya kuzima uasi
Sep 04, 2026 03:14Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Niger vimekamata hazina kubwa ya silaha na vifaa vya kijeshi baada ya kuzima uasi katika Kituo cha 101 huko Niamey, mji mkuu wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
-
Shambulio la RSF dhidi ya msafara wa misaada wa UN Kordofan Kusini, Sudan lauwa mtu 1 na kujeruhi 2
Sep 03, 2026 10:15Wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan wameshambulia msafara wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika jimbo la Kordofan Kusini, na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine wawili.
-
Umoja wa Afrika walaani hatua za kuvuruga amani nchini Niger
Sep 03, 2026 03:23Umoja wa Afrika (AU) umelaani jaribio la uasi wa kijeshi lililozimwa NCHINI Niger. Mwenyekiti wa Kamisheni ya umoja huo Mahmoud Ali Youssouf ameikosoa hatua hiyo na kuonya dhidi ya hatua yoyote ya kuchukua madaraka kwa kutumia nguvu.