Pars Today
Idadi ya vifo vilivyotokana na mripuko wa lori la petroli wiki iliyopita katika jimbo la Jigawa la kaskazini mwa Nigeria imeongezeka na kufikia watu 181.
Sudan imezishutumu nchi za Magharibi kwa kuingiza siasa katika suala la misaada ya kibinadamu na kulilaumu jeshi la Sudan na serikali ya nchi hiyo ya Kiarabu ya kaskazini mwa Afrika kwa 'kuzuia misaada.'
Kiongozi mwandamizi wa chama kimoja cha upinzani nchini Cameroon amesema jumuiya ya BRICS ni mbadala halisi wa kuleta mlingano kwenye jiopolitiki duniani na kusisitiza kwamba, nchi za Afrika zinaelewa fika suala hili.
Takriban raia 46 wameuawa huku wengine 44 wajeruhiwa katika siku mbili za mapigano kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha Radimali ya Haraka (RSF) katika majimbo ya Khartoum na Al-Jazira.
Baadhi ya vyombo vya habari vya Kenya vimeripoi kuwa, siasa za madai ya usaliti na njama za watu kuuawa zimeanza kujitokeza tena nchini humo baada ya naibu rais aliyetimuliwa mamlakani kudai alijaribiwa kulishwa sumu mara mbili.
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) limetangaza kuwa limefanikiwa kukomboa mji wa Kalembe ulioko katika mkoa wa Kivu Kaskazini kutoka kwa waasi wa M23.
Wataalamu wa mabadiliko ya tabia nchi wametahadharisha kuwa mgogoro wa hali ya hewa Afrika utawaelekeza katika umaskini watu wengine zaidi milioni 150 ifikapo mwaka 2050.
Rais William Ruto wa Kenya ameiomba Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi kadhaa za kupinga kuondolewa madarakani Rigathi Gachagua kama Naibu Rais, akisema kuwa masuala yaliyoibuliwa katika kesi hizo yametengewa Mahakama ya Juu pekee.
Waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya wamebaini "kubadilishwa bila sababu" kwa baadhi ya matokeo katika uchaguzi mkuu wa Msumbiji, huku kukiwa na shutuma za mgombea mkuu wa upinzani kwamba serikali ilimuua wakili wake.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa hatua madhubuti zinapasa kuchukuliwa ili kushughulikia mabadiliko ya tabianchi, migogoro na umaskini barani Afrika.