-
Jeshi la Mali: Makumi ya wanamgambo wameuawa karibu na Segou
Feb 09, 2026 06:42Jeshi la Mali limetangaza habari ya kufanya wimbi la mashambulizi yaliyoratibiwa ambayo yamewaua makumi ya washukiwa wa ugaidi, wakati wa operesheni zilizofanyika magharibi mwa jiji la Segou, katikati ya nchi.
-
Misri: Tunaunga mkono umoja wa ardhi ya Somalia na kupinga kuingilia masuala ya ndani ya mataifa mengine
Feb 09, 2026 03:09Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri amesema kuwa, Cairo inaunga mkono umoja wa ardhi ya Somalia na inasisitiza umuhimu wa ushiriki wake katika misheni ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika nchini humo.
-
Ethiopia yaitaka Eritrea iondoe haraka vikosi kwenye ardhi yake
Feb 09, 2026 03:07Serikali ya Ethiopia imeitaka nchi jirani ya Eritrea kuondoa haraka wanajeshi wake ambao inadai wako ndani ya eneo lake.
-
Tanzania: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu inaendelea tena leo
Feb 09, 2026 03:06Mahakama Kuu ya Tanzania imepanga kuendelea tena kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa upinzani Tundu Lissu. Ripoti zinasema, kesi hiyo inaendelea leo Jumatatu Februari 9 hadi Machi 6, 2026, mbele ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
-
Rais wa Somalia aapa kuzuia kambi ya kijeshi ya Israel katika eneo la Somaliland
Feb 08, 2026 23:29Rais wa Somalia amelaani vikali kile hatua ya utawala wa Israel kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake, akiahidi “kukabiliana” na uwepo wowote wa kijeshi wa Israel katika eneo la Somalia la Somaliland ambalo limejitangazia uhuru.
-
Kenya yaanza kuondoa askari Haiti huku kikosi kipya cha UN kikichukua hatamu
Feb 08, 2026 23:28Kenya itapunguza idadi ya maafisa wake wa polisi waliotumwa nchini Haiti baada ya kukamilisha jukumu lao kuu la kuleta uthabiti wa kiusalama. Hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Masuala ya Kigeni, Korir Sing’Oei.
-
Afrika Kusini kuondoa wanajeshi wake katika kikosi cha kulinda amani cha UN, nchini Kongo
Feb 08, 2026 05:42Afrika Kusini imesema kuwa itaondoa wanajeshi wake 700 waliokuwa wakihudumu katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO).
-
Waziri wa Habari wa Somalia: Hatutaruhusu Israel kutumia ardhi yetu kuwatishia majirani
Feb 08, 2026 05:10Waziri wa Habari, Utamaduni na Utalii wa Somalia, Daud Aweys Jama, amesema kwamba nchi yake imethibitisha mara kwa mara msimamo wake wa kupinga na kulaani ukiukaji wa wazi wa Israel wa mamlaka ya kujitawala Somalia na ardhi yake yote.
-
Katibu Mkuu wa UN alaani vikali kushadidi machafuko Sudan Kusini, ataka mapigano yasitishwe
Feb 08, 2026 02:47Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani vikali kushadidi kwa machafuko na mapigano nchini Sudan Kusini, ambako watu wapatao milioni 10, wakiwa ni zaidi ya theluthi mbili ya idadi ya watu wote nchini humo, wanahitaji msaada wa kibinadamu wa kuokoa maisha na wanaendelea kuathirika zaidi na mgogoro huo.
-
Tanzania, Uganda kuanza kuuza mafuta ghafi Julai mwaka huu
Feb 07, 2026 23:18Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema mafuta ghafi yatakayopita katika Mradi wa Bomba la Mafuta (EACOP) kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania yataanza kusafirishwa kwenda sokoni ifikapo Julai, mwaka huu.