Human Rights Watch yatahadharisha kuhusu kukandamizwa wapinzani Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i139738-human_rights_watch_yatahadharisha_kuhusu_kukandamizwa_wapinzani_tunisia
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) limelaani kile ilichokitaja kuwa ni ukandamizaji unaofanywa na mamlaka husika nchini Tunisia kwa wapinzani wa kisiasa na wanaharakati wa haki za binadamu.
(last modified 2026-07-09T03:11:44+00:00 )
Jul 09, 2026 03:04 UTC
  • HRW yakosoa ukandamizaji Tunisia
    HRW yakosoa ukandamizaji Tunisia

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) limelaani kile ilichokitaja kuwa ni ukandamizaji unaofanywa na mamlaka husika nchini Tunisia kwa wapinzani wa kisiasa na wanaharakati wa haki za binadamu.

Human Rights Watch pamoja na wataalamu wa Umoja wa Mataifa na makundi mengine ya asasi za kiraia yameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu mgogoro wa haki za binadamu unaozidi kuongezeka huko Tunisia.

Miaka mitano baada ya Rais wa Tunisia, Kais Saied, kujipatia mamlaka makubwa ya kiutendaji, hali ya haki za binadamu imeporomoka pakubwa  nchini humo.

Shirika  hilo la kutetea haki za binadamu limeongeza  kuwa utawala wa kimabavu ulioibuka upya Tunisia umekuwa ukikandamiza kimfumo wa asasi za kiraia, waandishi wa habari, wapinzani wa kisiasa, wanasheria huru, wahamiaji, na mmomonyoko wa utawala wa sheria.

Hivi karibuni mahakama nchini Tunisia zimewahukumu jela na kuwatoza faini kubwa watetezi wanane wa haki za binadamu kwa mashtaka yanayohusiana na kazi yao.

Katika kikao cha 62 cha Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, HRW imelitaka baraza hilo na nchi wanachama kuvunja ukimya wao na kulaani wazi ukandamizaji huo.