-
AU yataka Israel ishtakiwe kwa mauaji ya kimbari ya Ghaza na kutoshirikiana wala kuanzisha uhusiano nayo
Feb 17, 2025 03:39Wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika AU wametoa wito, mwishoni mwa mkutano wa 38 wa kilele uliofanyika mjini Addis Ababa, wa kusitishwa ushirikiano na kutoanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Maonyesho ya "Qur'ani katika Macho ya Wengine" yafunguliwa Tunisia
Feb 17, 2025 01:04Maonyesho ya "Qur'ani katika Macho ya Wengine" yamefunguliwa katika Maktaba ya Kitaifa ya Tunisia, na yataendelea hadi Aprili 30, kwa ushirikiano wa Taasisi ya Urithi wa Kitaifa na Taasisi ya Utafiti wa Kisasa wa Maghreb.
-
Waziri Mkuu wa zamani wa Mauritius akamatwa kwa tuhuma za utakatishaji pesa
Feb 16, 2025 23:37Waziri Mkuu wa zamani wa Mauritius Pravind Jugnauth amekamatwa na anakabiliwa na shtaka la utakatishaji pesa. Hayo yameelezwa na Tume ya Uhalifu wa Kifedha inayoendeshwa na serikali ya nchi hiyo.
-
Kumalizika mkutano wa 38 wa wakuu Umoja wa Afrika Addis Ababa
Feb 16, 2025 23:04Mkutano wa 38 wakuu wa Umoja wa Afrika ulimalizika jana katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa Ethiopia.
-
Katibu Mkuu wa UN aahidi Afrika kuwa na mwakilishi wa kudumu kwenye Baraza la Usalama
Feb 16, 2025 10:43Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema sio sawa kwa bara la Afrika kutokuwa na kiti cha mwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na ameahidi kufanya kazi na Umoja wa Afrika na nchi wanachama ili kuhakikisha kuwa nchi za Afrika zinapata mwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini: Tunapinga kufurushwa Wapalestina, hatutasalimu amri mbele ya vitisho vya Trump
Feb 16, 2025 10:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Ronald Lamola, amesema kuwa nchi za bara hilo zina msimamo mmoja juu ya haja ya kusuluhisha mgogoro wa Ukanda wa Gaza ndani ya suluhisho la mataifa mawili, akisisitiza kwamba Pretoria haitarudi nyuma kuhusiana na msimamo wake katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki.
-
Mkuu wa jeshi la Uganda atishia kuushambulia mji wa Bunia mashariki mwa Kongo
Feb 16, 2025 05:44Jenerali Muhoozi Kainerugaba Mkuu wa jeshi la Uganda jana aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kuwa nchi hiyo itaushambulia mji wa Bunia mashariki mwa Kongo iwapo wapiganaji wote katika eneo hilo hawatasalimisha silaha zao katika muda wa saa 24.
-
Odinga: Sina kinyongo, nimeridhishwa na matokeo ya uchaguzi wa AUC
Feb 15, 2025 23:23Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga amesema ameridhishwa na mchakato wa uchaguzi wa kumtafuta Mwenyekiti mpya wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), kurithi mikoba ya Moussa Faki Mahamat.
-
Al-Azhar yawataka Waarabu na Waislamu kupinga kufukuzwa Wapalestina Gaza
Feb 15, 2025 22:55Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar nchini Misri kimesisitiza kwa mara nyingine tena juu ya kupinga mpango wa kufukuzwa Wapalestina wa Gaza kutoka katika ardhi yao na kuwataka Waarabu na Waislamu kujitokeza na kupinga mpango huo.
-
Kesi 82 za madai ya watu kutoweka nchini Kenya zimeripotiwa tangu Juni 2024
Feb 15, 2025 22:52Nchini Kenya watu wanaituhumu polisi ya nchi hiyo kwa kufanya vitendo vya utekaji nyara lakini bado haijathibitishwa ni nani aliyehusika na utekaji huo.