Al-Azhar yawataka Waarabu na Waislamu kupinga kufukuzwa Wapalestina Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i122790-al_azhar_yawataka_waarabu_na_waislamu_kupinga_kufukuzwa_wapalestina_gaza
Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar nchini Misri kimesisitiza kwa mara nyingine tena juu ya kupinga mpango wa kufukuzwa Wapalestina wa Gaza kutoka katika ardhi yao na kuwataka Waarabu na Waislamu kujitokeza na kupinga mpango huo.
(last modified 2025-02-15T22:55:33+00:00 )
Feb 15, 2025 22:55 UTC
  • Al-Azhar yawataka Waarabu na Waislamu kupinga kufukuzwa Wapalestina Gaza

Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar nchini Misri kimesisitiza kwa mara nyingine tena juu ya kupinga mpango wa kufukuzwa Wapalestina wa Gaza kutoka katika ardhi yao na kuwataka Waarabu na Waislamu kujitokeza na kupinga mpango huo.

Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar nchini Misri kimetoa mwito kuungwa mkono misimamo ya Misri na mataifa mengine ya Kiarabu katika ujenzi na ukarabati mpya wa Ukanda wa Gaza bila ya kuondolewa wakazi wake.

Sehhemu nyingine ya taarifa ya al-Azhar imebainisha kwamba, inaunga mkono suala la kuijenga na kuikarabati Gaza, lakini kwa sharti kwamba Wapalestina wasalie katika eneo hilo na kuongezwa mashinikizo ya kutekelezwa makubaliano ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza.

Kadhalika  imewataka viongozi wote wa Kiarabu na Kiislamu kupinga mpango wa kuwafukuza Wapalestina, ambao imesema lengo lake kufuta kabisa kadhia ya  Palestina kwa kuwalazimisha Wapalestina kuondoka katika ardhi yao, ambayo wameishi kwa maelfu ya miaka.

Rais wa Marekani, Donald Trump, amekariri bila ya aibu pendekezo lake tata la kulinyakua na kulidhibiti eneo la Ukanda wa Ghaza, akisema amejitolea "kulinunua na kulimiliki" eneo hilo lililoharibiwa na vita uamuzi ambao umeibua upinzani mkali katika kila kona yay a ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu.