Semina ya kumuenzi Imam Shahidi Khamenei yafanyika nchini Tanzania
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i139702-semina_ya_kumuenzi_imam_shahidi_khamenei_yafanyika_nchini_tanzania
"Wakati wananchi nchini Iran wakifanya marasimu ya kuaga na mazishi ya mwili wa ‘Shahidi wa Iran’ Imam Khamenei, wapenzi wake nchini Tanzania pia waliandaa matukio mbalimbali ya maombolezo kwa ajili ya kuomboleza kifo cha shahidi cha Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu."
(last modified 2026-07-07T10:03:06+00:00 )
Jul 07, 2026 08:38 UTC
  • Semina ya kumuenzi Imam Khamenei yafanyika Tanzania
    Semina ya kumuenzi Imam Khamenei yafanyika Tanzania

"Wakati wananchi nchini Iran wakifanya marasimu ya kuaga na mazishi ya mwili wa ‘Shahidi wa Iran’ Imam Khamenei, wapenzi wake nchini Tanzania pia waliandaa matukio mbalimbali ya maombolezo kwa ajili ya kuomboleza kifo cha shahidi cha Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu."

Waislamu hao katika jiji Dar es Salaam wakiwa wamevaa mavazi meusi kama ishara ya huzuni walikusanyika na kumuomboleza kiongozi huyo wa mapinduzi ya Kiislamu ambaye leo mwili wake umeagwa katika mji mtakatifu wa Qom.

Zaidi ya waombolezaji 500 walishiriki katika semina kubwa ya kumbukumbu ya kumuenzi Kiongozi Shahidi, iliyofanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkutano huo, Sheikh Mullab Saleh Lulat alimsifu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei (r.a.), akisema kuwa alikuwa kiongozi aliyojitolea maisha yake yote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Sheikh Mullaba alieleza kuwa kiongozi huyo alikuwa mfano wa uongozi wa kweli wa kimungu, mwenye imani thabiti na uchamungu, ambaye alitumia uwezo na vipawa alivyokuwa navyo katika kuongoza watu kutoka kwenye giza kuelekea mwanga, kupigania ukombozi dhidi ya dhuluma na uonevu, na kushiriki kwa nafasi kubwa katika kuendeleza harakati ya muqawama.

Muhammad Javad Hematpanah, balozi wa Iran nchini Tanzania, pia katika hotuba yake alisisitiza imani kubwa ya Imam Shahidi kuhusu nafasi ya vijana katika kusukuma mbele malengo ya mfumo wa Kiislamu. Alisema mtazamo huu ulikuwa miongoni mwa sifa muhimu zaidi za uongozi wake na fikra zake za kutazamia mustakabali.

Mwisho wa hafla hiyo, washiriki walifanya maombolezo kwa ajili ya kuenzi kumbukumbu ya Imam Shahidi.

Aidha, katika hatua ya hiari ya wananchi, baadhi ya wapenzi na wafuasi wake waliweka picha kubwa za Kiongozi Shahidi pamoja na picha ya mfano ya ngumi yake iliyokunjwa kwenye mabango mbalimbali katika miji ya Tanzania."