-
Viongozi wa Umoja wa Afrika wakusanyika kwa mkutano muhimu Ethiopia
Feb 15, 2025 09:04Mkutano wa 38 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika umeanza leo Jumamosi katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, ukiwakutanisha pamoja viongozi wa mataifa kujadili masuala muhimu ya kikanda na bara, ikiwemo amani na usalama, ujumuishaji wa kiuchumi, na mageuzi ya kitaasisi.
-
Guterres aonya kuhusu uwezekano wa vita vya kikanda kutokana na mgororo wa DRC
Feb 15, 2025 08:58Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, leo Jumamosi amesisitiza umuhimu wa kuheshimu "mipaka" ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kuepusha vita vya kikanda.
-
Waasi wa M23 waingia Bukavu baada ya kutwaa uwanja wa ndege
Feb 15, 2025 03:42Waasi wa M23 wametangaza habari ya kuingia katika jiji la Bukavu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Wamorocco wafanya maandamano makubwa ya kuwaunga mkono Wapalestina
Feb 15, 2025 03:39Makumi ya maelfu ya wananchi wa Morocco wamejitokeza katika kona zote za nchi kushiriki maandamano ya kuunga mkono kadhia ya Palestina.
-
AU yatoa mwito wa kutatuliwa changamoto za kibinadamu na afya ya umma barani Afrika
Feb 14, 2025 23:12Kamishna wa Umoja wa Afrika (AU) wa Masuala ya Kibinadamu, Afya na Maendeleo ya Kijamii ametoa mwito wa kutafutwa ufumbuzi wa kudumu wa changamoto za afya ya umma na masuala ya kibinadamu barani Afrika.
-
UNHCR: Tulihudumia makumi ya maelfu ya wakimbizi mwaka 2024 nchini Libya
Feb 14, 2025 23:11Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limesema kwenye ripoti yake ya karibuni kabisa kwamba, mwaka uliopita wa 2024 lilihudumia makumi ya maelfu ya wakimbizi nchini Libya pekee ikiwa ni pamoja na kuwarejesha makwao mamia ya wengine.
-
Kikao cha mawaziri wa AU chamalizika kwa mwito wa maendeleo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii
Feb 14, 2025 09:30Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika wamemaliza Kikao chao cha 46 cha Kawaida cha Baraza la Utendaji la Umoja wa Afrika (AU) kwenye makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, Ethiopia na kutoa mwito wa kuendelea kupigania maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii barani humo.
-
Wanajeshi wa Ufaransa kutimuliwa pia nchini Senegal
Feb 14, 2025 09:02Ufaransa na Senegal zimeeleza kuwa zimeamua kuunda tume ikiwa ni katika fremu ya maandalizi ya kuondoka wanajeshi wa Ufaransa katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
-
Abuja yaijia juu Canada kwa kumyima 'viza' Mkuu wa Jeshi la Nigeria
Feb 14, 2025 08:40Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Nigeria, Jenerali Christopher Musa, ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya ubalozi wa Canada katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, kumnyima yeye na maafisa wengine wakuu wa kijeshi viza ya kwenda Canada kuhudhuria hafla ya michezo ya maveterani wa vita huko Vancouver.
-
Ugonjwa 'usiojulikana' waua makumi ya watu DRC; mapigano yanaendelea
Feb 14, 2025 08:40Ugonjwa usiojulikana umeua watu zaidi ya 50 katika eneo la Bansakusu, jimbo la Equateur, magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.