-
HRW: Serikali za Pembe ya Afrika zimeshindwa kulinda haki za raia
Jan 16, 2025 23:42Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limezituhumu serikali za nchi za Pembe ya Afrika kwa kushindwa kulinda haki za raia wao.
-
Jeshi la Sudan linachunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu
Jan 16, 2025 23:42Mkuu wa jeshi la Sudan ameunda kamati ya kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu uliofanywa wakati jeshi lake lililpoukomboa mji wa Wad Madani kutoka kwa wanamgambo wa Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF).
-
Viongozi wa Afrika wasisitiza ushirikiano katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Jan 16, 2025 07:36Viongozi wa nchi za Kiafrika wamesisitiza udharura wa kushirikiana nchi za bara hilo na kubuni tekolojia ya kukabiliana na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi ili kuhakikisha bara la Afrika linapata maendeleo endelevu.
-
Msumbiji yamwapisha rais mpya, ghasia za baada ya uchaguzi zaua watu 300
Jan 16, 2025 04:02Daniel Chapo wa chama tawala cha Frelimo jana Jumatano aliapishwa kuwa rais wa tano wa Msumbiji baada ya miezi kadhaa ya maandamano mabaya ambayo yamechukua roho za watu karibu 300 na kuwakosesha makazi mamia ya wengine.
-
UNICEF yapokea dola milioni 1.5 za kuwasaidia watoto wakimbizi wa Sudan walioko Libya
Jan 16, 2025 03:46Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) lilisema jana kwamba limepokea msaada wa dola milioni 1.5 kutoka kwa Shirika la Education Cannot Wait (ECW) ambao ni mfuko wa Umoja wa Mataifa wa elimu katika dharura. Msaada huo utatumika kushughulikia mahitaji ya dharura ya kielimu na kisaikolojia ya watoto wakimbizi wa Sudan walioko nchini Libya.
-
Miili ya watu 60 yatolewa kwenye mgodi wa dhahabu Afrika Kuisini; idadi isiyojulikana inahofiwa kufariki dunia
Jan 15, 2025 09:21Mamlaka ya Afrika Kusini imefanikiwa kupata miili 60 kutoka kwenye machimbo ya dhahabu yaliyogurwa huko Stilfontein, baada ya mzingiro wa wiki kadhaa uliolenga wachimbaji haramu.
-
Utafiti waonyesha kuwa Wakenya wana imani zaidi na viongozi wa dini kuliko asasi za Serikali
Jan 15, 2025 08:39Uchunguzi uliofanywa na shirika la utafiti Afrika la Afrobarometer umeonyesha kuwa, Wakenya sasa wana imani ya juu kwa viongozi wa dini na jeshi na hawana imani na wanasiasa pamoja na asasi za Serikali.
-
AU yapongeza mkutano wa viongozi wa Somalia na Ethiopia kufuatia mapatano ya Ankara
Jan 15, 2025 04:11Umoja wa Afrika umepongeza mkutano wa mwishoni mwa wiki kati ya viongozi wa Somalia na Ethiopia mjini Addis Ababa Ethiopia ambao ulifanyika kufuatia Azimio la Ankara.
-
WHO: Ugonjwa unaoshukiwa kuwa Marburg waua watu wanane Tanzania
Jan 15, 2025 00:27Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, mlipuko unaoshukiwa kuwa ni wa ugonjwa hatari wa Marburg nchini Tanzania umewaua watu wanane, na kuonya kwamba hatari ya kusambaa kwa ugonjwa huo nchini humo ni “kubwa”.
-
Besigye kushtakiwa katika Mahakama ya Kijeshi Uganda kwa kosa la uhaini lenye hukumu ya kifo
Jan 14, 2025 23:16Mahakama ya Kijeshi ya Uganda imetangaza kuwa, kiongozi mashuhuri wa upinzani nchini humo Daktari Kizza Besigye atafikishwa mahakamani kujibu shtaka zito la uhaini, ambalo linamuongezea matatizo ya kisheria mwanasiasa huyo kuelekea uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika 2026.