Ethiopia yaahidi kutumia fursa za biashara huria kutoa fursa zaidi barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i122512-ethiopia_yaahidi_kutumia_fursa_za_biashara_huria_kutoa_fursa_zaidi_barani_afrika
Waziri wa Biashara na Ushirikiano wa Kikanda wa Ethiopia amesema kuwa, nchi yake ina nia thabiti ya kuhakikisha kunakuwepo utekelezaji madhubuti wa makubaliano ya Eneo Huria la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) ili kutoa fursa kubwa za soko la ndani ya bara pana na kubwa la hilo.
(last modified 2025-02-09T07:09:52+00:00 )
Feb 09, 2025 07:09 UTC
  • Ethiopia yaahidi kutumia fursa za biashara huria kutoa fursa zaidi barani Afrika

Waziri wa Biashara na Ushirikiano wa Kikanda wa Ethiopia amesema kuwa, nchi yake ina nia thabiti ya kuhakikisha kunakuwepo utekelezaji madhubuti wa makubaliano ya Eneo Huria la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) ili kutoa fursa kubwa za soko la ndani ya bara pana na kubwa la hilo.

Waziri Yasmin Wohabrebbi amesema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa kukagua rasimu ya mkakati wa kitaifa wa utekelezaji ya AfCFTA na kuongeza kwamba, kuwa utekelezaji mzuri wa vipengee vya AfCFTA unatoa fursa kubwa za soko barani Afrika, kukuza uchumi wa viwanda, kuleta fursa za ajira nyingi na kuvutia uwekezaji.

Waziri wa Biashara na Ushirikiano wa Kikanda wa Ethiopia ameongeza kuwa nchi yake ina azma ya kuingia katika soko la ndani la Afrika ambalo halijatumiwa kwa kiasi kikubwa. Iwapo vipengee vya AfCFTA vitatekelezwa vizuri vitaleta fursa nyingi za maendeleo ya kiviwanda na upatikanaji wa malighafi muhimu za bara la Afrika ambazo hivi sasa zinayanufaisha madola ya nje ya bara hilo lenye utajiri mkubwa wa maliasili. Amesema kuwa, mkataba wa biashara huria wa bara la Afrika unatoa fursa ya kuchunguza uwezo wa masoko ya mataifa ya Afrika, kuzalisha utajiri mwingi na kufungua ukuaji wa viwanda.

AfCFTA ni mpango mkuu wa Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika. Lengo lake ni kuunda eneo kubwa zaidi la biashara huria duniani kulingana na idadi ya nchi zinazoshiriki. Tangu kuanza kutumika kwake mwaka 2019, nchi 47 za Afrika zimejiunga na mpango huo. Makubaliano ya AfCFTA yanalenga kukuza biashara ya ndani ya Afŕika kwa kuondoa vikwazo vya biashaŕa. AfCFTA ina watu bilioni 1.4 na jumla ya pato la ndani ni dola trilioni 3.4 na ina uwezo wa kubuni ajira, kukuza thamani za bidhaa za kikanda, kuvutia uwekezaji na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kote Afrika.