-
Afrika Kusini yatangaza janga la kitaifa kufuatia mvua na mafuriko yaliyouwa watu 30
Jan 19, 2026 08:05Afrika Kusini imetangaza janga la kitaifa kutokana na mvua kubwa na mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya takriban watu 30 kaskazini mwa nchi hiyo, kuharibu maelfu ya nyumba na kusomba barabara na madaraja.
-
Nigeria yauwa magaidi 40 wa Boko Haram katika operesheni za anga
Jan 19, 2026 08:04Jeshi la Anga la Nigeria limetangaza kuwua limeuwa takriban magaidi 40 wa Boko Haram katika mashambulizi ya anga mtawalia iliyofanya mapema wiki hii katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria.
-
Rached Ghannouchi Kiongozi wa Ennahda Tunisia atimiza siku 1,000 jela
Jan 19, 2026 08:00Rached Ghannouchi kiongozi wa chama cha Kiislamu chenye ushawishi mkubwa nchini Tunisia cha al-Nahdha na Spika wa zamani wa bunge la nchi hiyo jana Jumapili alitimiza siku 1,000 akiwa kifungoni jela. Ghannouchi ametaja kifungo kinachomkabili kuwa ni " wakati wa mahesabu ya kisiasa."
-
Afisa wa UN: Sudan 'imetumbukia katika shimo la mateso makubwa yasiyoelezeka'
Jan 19, 2026 03:50Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ametahadharisha kuhusu kuzorota kwa hali ya haki za binadamu na kibinadamu nchini Sudan, kufuatia ziara yake ya siku tano katika nchi hiyo inayokumbwa na vita.
-
Umoja wa Afrika kufufua mchakato wa amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Jan 19, 2026 03:48Viongozi wa Kiafrika na wa kimataifa waliokutana mjini Lomé wamekubaliana kuimarisha na kuunganisha juhudi za upatanishi ili kumaliza mzozo katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mkutano huo umeidhinisha nafasi ya kiungo ya upatanishi unaoongozwa na Togo chini ya mamlaka ya Umoja wa Afrika (AU), kama mhimili mkuu wa kusukuma mbele mchakato wa amani.
-
Rais Doumbouya wa Guinea ameapa kutotumia madaraka kwa manufaa yake binafsi
Jan 18, 2026 23:15Rais wa Guinea aliyeapishwa hivi karibuni, Mamady Doumbouya, ameahidi kutotumia vibaya madaraka yake ya urais, akisema ‘‘hatatumia kamwe mamlaka’’ aliyopewa ‘’kwa ajili ya maslahi binafsi’’.
-
Rais wa Somalia atoa wito kwa Somaliland kushiriki katika mazungumzo
Jan 18, 2026 09:05Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amewatolea wito maafisa wa Somaliland kushiriki katika mazungumzo na serikali yake; akisema kuwa yuko tayari kuafikiana katika masuala yote isipokuwa "umoja wa nchi."
-
Uchaguzi Uganda; Bobi Wine apinga ushindi wa Museveni
Jan 18, 2026 06:56Kiongozi wa upinzani na mshindani mkuu wa Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi mkuu wa hivi karibuni nchini Uganda, Robert Kyangulani maarufu kama Bobi Wine amesema hakubaliani na matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo.
-
Watu wanane wafa, 20 wajeruhiwa, makumi ya nyumba zateketea kwa moto, Kibera nchini Kenya
Jan 18, 2026 02:16Taarifa za awali zinasema kuwa watu wasiopungua wanane wamepoteza maisha na wengine zaidi ya ishirini wamejeruhiwa baada ya moto mkubwa kuzuka katika eneo la Makina la makazi duni ya watu huko Kibera, Kaunti ya Nairobi nchini Kenya.
-
Doumbouya, kiongozi wa kijeshi aliyegombea urais na kushinda aapishwa kuwa rais wa Guinea
Jan 17, 2026 23:40Mamady Doumbouya, jenerali aliyeongoza jeshi la Guinea kuchukua madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi mnamo mwaka 2021, ameapishwa kuwa rais wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.