-
DR Kongo: Rwanda Inavuruga GPS na kutekeleza hujuma mtandaoni
Jul 30, 2024 23:34Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeituhumu nchi jirani ya Rwanda kwa kukwamisha mfumo wa uongozaji kwa satelaiti duniani (GPS) mashariki mwa Kongo na kufanya mashambulizi ya mtandaoni "yenye lengo la uvurugaji".
-
HRW: Pande hasimu Sudan zimeshiriki katika ukatili mkubwa wa kijinsia
Jul 29, 2024 22:59Pande zinazozozana huko Sudan zimeshiriki katika ukatili mkubwa wa kingono na kijinsia katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.
-
Baraza Kuu la Waislamu Kenya launga mkono mazungumzo ya kitaifa
Jul 29, 2024 10:58Baraza Kuu la Waislamu Nchini Kenya (SUPKEM) limeunga mkono mazungumzo kuhusu masuala ambayo yameibuliwa vijana wanaofanya maandamano dhidi ya serikakli ya Rais William Ruto maarufu kama na Gen Z ili kukomesha zogo la kisiasa linaloendelea kushuhudiwa nchini humo.
-
Zuma kushirikisha timu ya wanasheria baada ya kufukuzwa katika chama tawala cha ANC
Jul 29, 2024 09:20Chama cha uMkhonto weSizwe cha nchini Afrika Kusini kimesema kuwa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Jacob Zuma, atashirikisha timu yake ya mawakili kumtetea kufuatia hatua ya chama tawala cha ANC ya kumfukuza chamani baada ya chombo kimoja cha habari nchini humo kuweka wazi waraka uliovuja.
-
DRC yaanza kuachia huru wafungwa kupunguza msongamano katika jela kuu ya Kinshasa
Jul 28, 2024 23:25Wafungwa wapatao 7,000 wataachiliwa huru kwa masharti kutoka kwenye jela kuu ya Makala iliyoko katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kinshasa katika jitihada za kupunguza msongamano wa wafungwa wanaoshikiliwa katika jela hiyo.
-
Mahakama ya Nigeria yawatia hatiani wanamgambo 125 wa kundi la kigaidi la Boko Haram
Jul 28, 2024 23:03Mahakama nchini Nigeria imewatia hatiani wanamgambo 125 wa kundi la kigaidi la Boko Haram na wafadhili wa kifedha wa msururu wa makosa yanayohusiana na ugaidi.
-
Shambulio la RSF laua watu 22 el-Fasher, magharibi mwa Sudan
Jul 28, 2024 03:23Kwa akali watu 22 wameuawa katika shambulio linalodaiwa kufanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika mji wa el-Fasher, jimboni Darfur, magharibi mwa Sudan.
-
Wanajeshi wa Uganda na DRC waokoa watu wengine 23 waliotekwa nyara na waasi wa ADF
Jul 27, 2024 23:45Wanajeshi wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana Jumamosi walifanikiwa kuokoa watu wengine 23 waliotekwa nyara na waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) katika operesheni yao ya pamoja ya kijeshi mashariki mwa DRC.
-
Muuaji hatari aaga dunia huku waathiriwa wakiendelea kudai haki
Jul 27, 2024 23:43Louis van Schoor, muuaji wa halaiki aliyepatikana na hatia nchini Afrika Kusini na ambaye anayejulikana kwa jina la "Apartheid Killer", amefariki dunia.
-
Wananchi wa Tunisia wataka kufukuzwa balozi wa Marekani nchini mwao
Jul 27, 2024 23:43Mamia ya raia wa Tunisia wameandamana na kukusanyika mbele ya ubalozi wa Marekani nchini humo, wakipinga kuendelea kuuawa kwa raia katika Ukanda wa Gaza.