-
Rais wa DRC amkosoa mwenzake wa Kenya kwa 'kuushughulikia vibaya' Mchakato wa Nairobi
Jul 27, 2024 08:04Rais Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amemkosoa mwenzake wa Kenya William Ruto kwa alichokiita kushughulikia vibaya Mchakato wa Nairobi, ambao ulibuniwa kuanzisha mazungumzo na makundi yenye silaha mashariki mwa DRC. Tshisekedi amemshutumu Ruto kuwa anaegemea upande wa Rwanda, msimamo anaoamini umekwamisha mpango huo.
-
Mvua kubwa yazidisha mateso ya wakimbizi mashariki mwa Sudan
Jul 27, 2024 03:32Mvua kubwa inayoendelea kunyesha huko mashariki mwa Sudan imezidisha mateso ya watu waliokimbia makazi yao haswa katika miji ya Gedaref, Kassala na Halfa Aj Jadeedah.
-
Ethiopia yaanza siku 3 za maombolezo baada ya maporomoko ya udongo kuua 260
Jul 26, 2024 23:59Bunge la Ethiopia limetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo Jumamosi kufuatia maporomoko ya udongo yaliyoua mamia ya watu.
-
Walibya 95 wakamatwa Afrika Kusini katika kambi ya kijeshi inayoshukiwa
Jul 26, 2024 22:55Polisi nchini Afrika Kusini imetangaza kuwa, siku ya Ijumaa Julai 26 iliwakamata Walibya 95 baada ya kuvamia shamba ambalo linaonekana kutumika kama kambi ya kijeshi.
-
Burundi yatangaza maambukizo ya kwanza ya MPOX
Jul 26, 2024 22:54Waziri wa afya wa Burundi ametangaza kuwa, kumesajiliwa visa vya kwanza vya ugonjwa wa homa ya nyani, Mpox nchini humo, hali ambayo imezusha hofu kwamba kirusi hicho kipya na kikali zaidi kimevuka mpaka na kuingia nchini humo kikotokea nchii jirani.
-
Maelfu ya watoto Kusini mwa Afrika wanakabiliwa na utapiamlo
Jul 26, 2024 04:14Ukame mkali ambao umeathiri maeneo makubwa ya Kusini mwa Afrika na unatishia maisha ya mamia ya maelfu ya watoto katika nchi sita zilizoathiriwa zaidi.
-
Wimbi la joto kali laua watu 21 nchini Morocco
Jul 25, 2024 23:58Vifo 21 vimeripotiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Beni Mellàl katikati mwa Morocco kutokana na wimbi la joto kali.
-
Umoja wa Mataifa na viongozi wa Afrika watoa mwito kwa juhudi za pamoja ili kufikia SDGs
Jul 25, 2024 23:48Maafisa wa Umoja wa Mataifa, wataalamu na wachukua maamuzi wanaohudhuria mkutano wa ngazi za juu unaomalizika leo Ijumaa mjini Addis Ababa Ethiopia na ambao unahusu maendeleo endelevu, wametoa mwito wa kufanyika marekebisho ya haraka katika mfumo wa fedha wa kimataifa ili kurahisisha kufikiwa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ifikapo mwaka 2030.
-
Wanachama 300 wa Boko Haram wapandishwa kizimbani "kwa mpigo" nchini Nigeria
Jul 25, 2024 23:47Kesi ya halaiki ya wanachama 300 wa genge la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram imeanza kusikilizwa kwa mkupuo mmoja nchini Nigeria.
-
Mkutano wa Djibouti waonya juu ya hali ya mbaya na kodorora usalama nchini Sudan
Jul 25, 2024 07:25Mkutano wa pili wa mashauriano kuhusu jinsi ya kuimarisha uratibu wa mipango na juhudi za amani nchini Sudan umetahadharisha kuhusu athari za hali tata ya kibinadamu na usalama nchini Sudan, ukitoa wito wa kusitishwa mapigano, kuimarishwa mazungumzo ya kisiasa na kurejeshwa amani na utulivu nchini humo.