Muuaji hatari aaga dunia huku waathiriwa wakiendelea kudai haki
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i114548-muuaji_hatari_aaga_dunia_huku_waathiriwa_wakiendelea_kudai_haki
Louis van Schoor, muuaji wa halaiki aliyepatikana na hatia nchini Afrika Kusini na ambaye anayejulikana kwa jina la "Apartheid Killer", amefariki dunia.
(last modified 2024-07-27T23:43:31+00:00 )
Jul 27, 2024 23:43 UTC
  • Muuaji hatari aaga dunia huku waathiriwa wakiendelea kudai haki

Louis van Schoor, muuaji wa halaiki aliyepatikana na hatia nchini Afrika Kusini na ambaye anayejulikana kwa jina la "Apartheid Killer", amefariki dunia.

Mzee huyo wa miaka 72 alikuwa hospitalini akiwa na maambukizi kwenye mguu wake. Binti yake aliiziambia duru za habari kwamba, baba yake alifariki dunia siku ya Alkhamisi "kutokana na maambukizi ya bakteria".

Kifo cha Van Schoor kinatokea chini ya wiki moja baada ya uchunguzi duru za habari kuhusu maisha yake ya zamani, ambao ulifichua maelezo mapya ya kutisha kuhusu mfululizo wa mauaji aliyotekeleza mwishoni mwa miaka ya 1980 katika miaka ya mwisho ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Dada ya mmoja wa waathiriwa wake amesema, anatumai polisi watafungua upya kesi hizo kwa uchunguzi licha ya kifo chake.

Wakati ambapo mfumo wa kibaguzi uliweka uongozi mkali uliowapa upendeleo Waafrika Kusini weupe, Van Schoor alikuwa akifanya kazi kama mlinzi wa binafsi katika jiji la pwani la London Mashariki.

Kati ya 1986 na 1989, alipiga risasi na kuua watu wasiopungua 39. Waathiriwa wake wote walikuwa Waafrika wazalenzo na mdogo alikuwa na miaka 12 tu.