Havana yatahadharisha: Mashambulizi ya Marekani dhidi ya Cuba yatasababisha umwagaji damu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i138352-havana_yatahadharisha_mashambulizi_ya_marekani_dhidi_ya_cuba_yatasababisha_umwagaji_damu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba ametahadharisha kuwa: Hujuma yoyote ya kijeshi ya Marekani dhidi ya nchi hiyo itasababisha maafa ya binadamu na umwagaji damu.
(last modified 2026-05-14T10:16:35+00:00 )
May 14, 2026 10:13 UTC
  • Bruno Rodriguez Parrilla
    Bruno Rodriguez Parrilla

Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba ametahadharisha kuwa: Hujuma yoyote ya kijeshi ya Marekani dhidi ya nchi hiyo itasababisha maafa ya binadamu na umwagaji damu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Bruno Rodriguez Parrilla ameeleza katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii kwamba: "Raia wa Cuba na Marekani watauawa iwapo Marekani itaishambulia Cuba; na ni wanasiasa wale ambao tu hawawatumi watoto na familia zao vitani wanaoweza kuthubutu kuchukua hatua kama hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba ameongeza kuwa: "Hakuna kabisa sababu au kisingizio kidogo kabisa cha kuifanya Marekani ianzishe mashambulizi katika kisiwa kidogo ambacho hakina tishio lolote, kwa sababu tu watu wachache wanataka kubadilisha mfumo wa kisiasa au serikali ya Cuba."

Hivi karibuni, na wakati huo huo kwa mujibu wa ripoti ya tovuti ya NBC kwamba Rais wa Marekani Donald Trump amekasirishwa na uwezo wa Cuba wa kuhimili mashinikizo ya Washington, tovuti ya Marekani ya Axios imetangaza kuwa kuna uwezekano Marekani hivi karibu ikakishambulia kisiwa hicho cha Karibiani.

Kwa zaidi ya miongo sita sasa, Cuba imekuwa chini ya vikwazo vikubwa na visivyo vya kibinadamu vya Marekani, ambavyo ni ukiukaji wa wazi wa kanuni za kimsingi za Mkataba wa Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa.