Kukaribia mwisho wa kisiasa wa Starmer na kuzidi kupata nguvu Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i138334-kukaribia_mwisho_wa_kisiasa_wa_starmer_na_kuzidi_kupata_nguvu_iran
Pars Today - Magazeti ya Uingereza yameripoti kwa wingi habari inayosisitiza kuwa, kusambaratika kisiasa Waziri mkuu wa nchi hiyo Keir Starmer kumekaribia.
(last modified 2026-05-14T05:55:33+00:00 )
May 13, 2026 18:54 UTC
  • Kukaribia mwisho wa kisiasa wa Starmer na kuzidi kupata nguvu Iran

Pars Today - Magazeti ya Uingereza yameripoti kwa wingi habari inayosisitiza kuwa, kusambaratika kisiasa Waziri mkuu wa nchi hiyo Keir Starmer kumekaribia.

Hii ni kwa sababu mgogoro wa kisiasa nchini Uingereza umeingia katika awamu mpya kwa Keir Starmer, Waziri Mkuu na kiongozi wa Chama cha Labour huku vyombo vya habari vikubwa zaidi nchini humo vikiripoti kuongezeka mashinikizo ya kumtaka ajiuzulu. Wimbi la maandamano na malalamiko limeibuka ndani ya chama cha Labour baada ya kushindwa vibaya chama hicho katika uchaguzi wa madiwani na kupoteza zaidi ya viti 1,000 hadi 1,400. Magazeti makubwa ya Uingereza, ikiwa ni pamoja na The Times, The Telegraph, The Guardian, The Daily Express, na BBC, yameandika katika ripoti zao kwamba wawakilishi kadhaa wa Chama cha Labour wanamnyooshea kidole cha lawama moja kwa moja Starmer kwa kushindwa vibaya chama hicho huku wakitaka ratiba ya kuondoka kwake madarakani na ndani ya chama na serikali itangazwe haraka. Baadhi ya ripoti zimesema kuwa idadi ya wabunge ambao wamemtaka Starmer ajiuzulu; hadharani au faraghani ni kati ya miaka 70 na zaidi ya 80.

Wakati huo huo, gazeti la The Times la nchini Uingereza limeripoti kwamba Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Shabana Mahmood na mawaziri wengine wawili wakubwa wa Uingereza wamemtaka Keir Starmer atangaze ratiba ya kujiuzulu kwake.

Wakati huo huo, Shirika la Utangazaji la kifalme la Uingereza yaani BBC limeripoti kwamba Tom Rutland na Joe Morris, manaibu wawili wa Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, wamejiuzulu na kumtaka Starmer kuchukua hatua kama hiyo.

Lakini pia katika hotuba yake ya hivi karibuni iliyolenga "kuirejesha" serikali na kudhibiti mgogoro wa ndani ya Chama cha Labour, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, alishindwa kuwatuliza wapinzani wake na amekumbwa na wimbi kubwa la ukosoaji. Wawakilishi wa Chama cha Labour na viongozi kadhaa wa vyama vya wafanyakazi waliitaja hotuba ya Starmer kuwa "haitoshi" na "haina mpango wa wazi wa utekelezaji," na wanaamini kwamba hotuba hiyo ilishindwa kurejesha imani iliyopotea.

Huku migogoro ya kisiasa ikiongezeka huko Uingereza na Marekani, vyombo vya habari vya Lebanon vimekiri kwamba baada ya vita vya Ramadhani sasa Iran imekuwa taifa kubwa duniani.

Vyombo hivyo vya habari vimefichua uongo wa rais wa Marekani kuhusu Iran na kuandika kuwa, tofauti na propaganda za uongo za Trump, Iran imekuwa taifa kubwa la kikanda na pia imebadilisha mlingano wa nguvu duniani.

Gazeti la la Al-Ahed la Lebanon limeandika makala yenye kichwa cha maneno "Kwa nini Merakani imebaki peke yake katika Lango Bahari la Hormuz" kwamba: Baada ya Vita vya Pili vya Dunia Marekani ililazimisha ionekane kuwa ndiye polisi wa dunia na inaweza kufanya chochote bila ya kupingwa. Lakini taarifa za hivi karibuni za Waziri wa Vita wa Marekani Pete Hegseth na ujumbe wa Donald Trump kwenye mtandao wake wa kijamii vyote vinaonesha kushindwa Marekani kukabiliana na Iran katika Lango Bahari la Hormuz.

Limeandika: Kwa kweli, mataifa ya Ulaya hayakusimama upande wa Wamarekani na washirika wao wengine. Hii ndiyo inayoitwa "kushindwa kimkakati" baada ya dola linalojifanya ni kubwa, kutoweza kutekeleza kivitendo vitisho vyake. Kuendelea kulegeza misimamo Marekani kwa kisingizio cha mazungumzo ya kidiplomasia, kwa kweli, ni kukiri waziwazi Washington kwamba imesusiwa kimataifa.

Vyombo vya habari vya Lebanon aidha vimeandika: Ikumbukwe kwamba enzi ambazo Marekani ilifanya kazi peke yake kama polisi wa dunia zimekwisha. Ulaya imeonesha kivitendo kwamba vita vya Asia Magharibi kwake ni mstari mwekundu na haikukubali tena kuburuzwa na Washington. Matokeo yake, Marekani imelazimika kurudi nyuma na kulegeza kamba katika mzozo ambao ilihitaji mno kushinda, na imepata hasara kubwa tena bila ya mafanikio yoyote ya kimkakati.

Amma somo lililopatikana duniani ni kwamba, kila nchi lazima ilipe gharama ya kijeshi kwa mujibu wa ilivyojizatiti na kwa maamuzi yake inayochukua. Muhimu ni kwamba; kila nchi lazima iwe na nguvu ili kuhakikisha ina nafasi muhimu ndani na nje ya mipaka yake.

Gazeti la Al-Ahed la Lebanon limeandika: Baada ya siku arobaini za uvamizi wa Marekani na Wazayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dunia imeona kwamba Iran si nchi ya kuchezewa na hilo ndilo lililoahidiwa na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, leo hii Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imebadilisha mlingano wa nguvu duniani na imekuwa taifa kubwa ulimwenguni, ikisimama kidete mbele ya nguvu ambazo huko nyuma zilikuwa zinaamini kwamba zinaweza kufanya chochote duniani. Kwa hakika Iran imesambaratisha mpango wa kibeberu wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa kutaka kuzidhibiti nchi za dunia.