Bolton: Trump amenaswa katika mtego wa kujitengenezea wa Iran
-
John Bolton
Mshauri wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Marekani amesema: Donald Trump, Rais wa nchi hiyo, amenaswa katika mtego wa kujitengenezea mwenyewe wa Iran.
Katika makala aliyoandika kwenye gazeti la Washington Post, John Bolton, amekosoa vikali sera za Donald Trump kuhusu vita dhidi ya Iran na kusema: "Trump amenaswa katika mtego. Kwa upande mmoja, ana kiu ya kufikia makubaliano ambayo anaweza kuyaita "ushindi", na kwa upande mwingine, anaogopa sana kusaini makubaliano sawa na JCPOA na kukosolewa."
Bolton pia ameonya kwamba ikiwa vita dhidi ya Iran vitaisha kidiplomasia, basi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaweza kutumia suala hilo, kama "kitufe cha kuwashia taa", kuzidisha au kupunguza mashinikizo kwa uchumi wa dunia wakati wowote inapotaka.
Mshauri wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Marekani ameongeza kuwa: Trump alianzisha vita dhidi ya Iran, lakini sasa anaogopa na kubakia bumbuazi.