Madaktari wa magonjwa ya akili wa Marekani: Trump anapasa kuuzuliwa mamlakani
-
Donald Trump
Makumi ya madaktari wa magonjwa ya akili na wataalam wakuu wa afya ya akili nchini Marekani wametia saini taarifa ambayo imemtaja Rais Donald Trump kuwa "hatari ya wazi na ya haraka" na kutaka hatua za haraka zichukuliwe ili kumuondoa madarakani.
"Madaktari thelathini wa madaktari wa magonjwa ya akili na wataalam wa afya ya akili wa Marekani walitia saini taarifa wakisema kwamba Donald Trump hawezi kiakili kuendelea kuwa rais na kwamba kuwa kwake na mamlaka ya kudhibiti silaha za nyuklia za Marekani kunaweza kuwa hatari kwa dunia nzima."
Madaktari hao wa Marekani wamegundua kuwa, kupungua kwa kiasi kikubwa uwezo wa kutambua na kuchanganua mambo, kusinzia mara kwa mara waziwazi mbele ya hadhara muhimu ya umma, kuchanganyikiwa pakubwa katika kuchukua maamuzi, kushindwa kujizuia kuchukua hatua, kujiona kuwa mtu mwenye mamlaka na uwezo wa aina yake kuliko wengine ni miongoni mwa sifa za Trump.