-
WFP kusimamisha huduma ya msaada wa chakula nchini Somalia
Feb 21, 2026 22:46Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetangaza kuwa, huenda likasitisha msaada na harakati zake za kibinadamu nchini Somalia ifikapo mwezi Aprili mwaka huu sababu ni ufadhili mpya kutopatikana haraka.
-
WHO: Makumi ya watu wameuawa katika mashambulio dhidi ya vituo vya afya Sudan
Feb 21, 2026 22:45Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, makumi ya watu wameuawa kufuatia mashambulio dhidi ya vituo vya afya nchini Sudan.
-
Afisa wa EU awashinikiza waasi wa DR Congo kufungua njia za kibinadamu
Feb 21, 2026 22:45Kamishna wa Umoja wa Ulaya, anayehusika na masuala ya misaada ya kibinadamu, amewasihi waasi wa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufungua njia za kibinadamu kwa ajili ya kupata misaada mamilioni ya raia mashariki mwa nchi hiyo inayokabaliwa na machafuko.
-
Shirikisho la Soka Senegal lapinga hukumu ya mashabiki wao Morocco
Feb 21, 2026 22:44Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) limelaani hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Morocco dhidi ya mashabiki 18 wa Senegal waliopatikana na hatia ya kufanya vurugu kufuatia fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON.
-
Kenya yaitaka Russia iirejeshee miili na raia wake waliofungwa katika vita vya Ukraine
Feb 21, 2026 07:37Serikali ya Kenya imeitaka Russia iirejeshe nyumbani miili ya raia wake waliouawa na wale waliokamatwa kama wafungwa wa vita, ambao wameripotiwa kuwa walipiigania Russia katika vita na Ukraine.
-
Watu 50 wauawa katika shambulio la wabeba silaha kaskazini magharibi ya Nigeria
Feb 21, 2026 07:36Kundi moja la wabeba silaha limewaua watu wasiopungua 50 na kuwateka nyara wanawake na watoto katika shambulio la usiku kwenye kijiji kimoja kilichoko kaskazini magharibi mwa Jimbo la Zamfara nchini Nigeria.
-
Guinea-Bissau yasitisha utafiti wa chanjo unaofadhiliwa na Marekani
Feb 21, 2026 04:07Guinea-Bissau imesitisha utafiti tata wa chanjo ya homa ya ini aina ya B (Hepatitis B) uliokuwa ukifadhiliwa na utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump, baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kueleza wasiwasi mkubwa wa kimaadili kuhusu muundo wa utafiti huo.
-
WFP: Somalia inakabiliwa na hatari ya baa la njaa
Feb 21, 2026 04:06Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP limesema hali ya upatikanaji wa chakula nchini Somalia imefikia hatua mbaya ambapo mamilioni ya watu wako hatarini kukumbwa na njaa kali kutokana na ukosefu wa fedha za msaada.
-
Al-Burhan: Hakutakuwa na suluhu Sudan mpaka RSF iondoke kwenye maeneo yote inayoyakalia
Feb 20, 2026 22:53Mkuu wa Baraza la Utawala la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, amesema hakutakuwa na usitishaji mapigano mpaka pale Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) vitakapojiondoa kwenye kile alichokieleza kuwa ni maeneo vinayoyakalia na kujikusanya upya katika maeneo yaliyotengwa.
-
Mashabiki 18 wa Senegal wahukumiwa vifungo jela Morocco kwa yaliyojiri kwenye fainali ya AFCON
Feb 20, 2026 22:52Mahakama ya Morocco imewahukumu mashabiki 19 wa soka kifungo cha mwaka mmoja jela kwa vitendo vya kihuni walivyovionesha wakati wa mchezo wa fainali ya AFCON 2025 kati ya Morocco na Senegal, ambapo walijaribu kuvamia uwanja.