Afisa wa EU awashinikiza waasi wa DR Congo kufungua njia za kibinadamu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i136890-afisa_wa_eu_awashinikiza_waasi_wa_dr_congo_kufungua_njia_za_kibinadamu
Kamishna wa Umoja wa Ulaya, anayehusika na masuala ya misaada ya kibinadamu, amewasihi waasi wa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufungua njia za kibinadamu kwa ajili ya kupata misaada mamilioni ya raia mashariki mwa nchi hiyo inayokabaliwa na machafuko.
(last modified 2026-02-22T02:15:01+00:00 )
Feb 22, 2026 02:15 UTC
  • Afisa wa EU awashinikiza waasi wa DR Congo kufungua njia za kibinadamu
    Afisa wa EU awashinikiza waasi wa DR Congo kufungua njia za kibinadamu

Kamishna wa Umoja wa Ulaya, anayehusika na masuala ya misaada ya kibinadamu, amewasihi waasi wa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufungua njia za kibinadamu kwa ajili ya kupata misaada mamilioni ya raia mashariki mwa nchi hiyo inayokabaliwa na machafuko.

Hadja Lahbib Kamishna wa Umoja wa Ulaya, anayehusika na masuala ya misaada ya kibinadamu, alihitimisha ziara yake katika eneo la Maziwa Makuu siku ya Ijumaa, Februari 20.

Lahbib alikutana na viongozi wa Alliance Fleuve Congo (AFC/M23), muungano wa waasi mashariki mwa Kongo unaowajumuisha waasi wa M23, huko Goma, kama sehemu ya ziara yake ya kikanda, ambayo ilimpeleka Rwanda na Burundi.

"Nilikuja Goma na agizo la kibinadamu. Nilikuwa na mkutano wa wazi na wenye kujenga na wawakilishi wa AFC/M23 ili kuhimiza upatikanaji wa kibinadamu kwa mamilioni ya raia mashariki mwa DRC. Misaada lazima iwafikie wale wanaohitaji bila kuchelewa, kupitia njia salama za kibinadamu," aliwaambia waandishi wa habari.  Aidha alisema: "Sheria ya Kimataifa ya Kibinadamu lazima iheshimiwe ili kuwalinda raia.

Aidha alihitimisha ziara yake huko Goma, jiji kuu mashariki mwa DRC baada ya kukutana na Marais Félix Tshisekedi wa DRC, Évariste Ndayishimiye wa Burundi, na Paul Kagame wa Rwanda.

Mwishoni mwa mkutano huo, Hadja Lahbib alionyesha kwamba, ahadi zilikuwa zimetolewa, haswa kuhusu ufikiaji wa kibinadamu. "Nilipata ahadi thabiti kutoka kwa pande zote nilizokutana nazo. Natumai zitatekelezwa na kwamba misheni hii itazaa matunda," alisema wakati wa hotuba yake.