-
Gabon inamshikilia Waziri wake wa utalii kwa madai ya ufisadi wa dola milioni 18
Dec 04, 2025 00:14Pascal Ogowé Siffon Waziri wa Utalii wa Gabon amewekwa katika kifungo cha nyumbani baada ya kukamatwa. Hatua hii imechukuliwa baada ya Waziri huyo wa Utalii wa Gabon kujaribu kuondoka Libreville.
-
Libya: Tutawatendea wakimbizi wa Sudan kama Walibya, watapatiwa huduma za skuli na hospitali
Dec 03, 2025 07:24Serikali ya Libya imetangaza kuwa itaongeza kasi ya kuwarejesha makwao wahamiaji wasio halali wa Kiafrika wa nchi za chini ya Jangwa la Sahara, lakini imesema, kwa upande wa wakimbizi wa Sudan watachukuliwa kama Walibya na kuruhusiwa kupata huduma za skuli na hospitali.
-
Je, kujitawala kiuchumi Niger kutakuwa pigo la mwisho kwa ukoloni wa Ufaransa barani Afrika?
Dec 03, 2025 05:44Niger imeanza kuuza urani yake katika soko la kimataifa baada ya kukata mkono wa Ufaransa katika sekta ya madini hayo nchini humo.
-
Umoja wa Mataifa: El Fasher Sudan kumefanyika jinai za kivita
Dec 03, 2025 03:06Mratibu wa Msuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan amesema mapema leo Jumatano kwamba maeneo mengi ya makazi ya raia nchini humo yamezingirwa na haiwezekani kuyafikishia misaada.
-
Mapigano yashadidi DRC, kila upande unamtuhumu mwenzake
Dec 03, 2025 03:05Mapigano yamezidi kupamba moto mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku jeshi na waasi wa M23 kila upande ukimshutumu mwenzake kwa kukanyaga makubaliano ya kusitisha mapigano.
-
UNHCR: Watu 100,000 wamekimbia Kaskazini mwa Msumbiji huku machafuko yakishadidi
Dec 02, 2025 23:18Watu takribani 100,000 wamelazimika kuyakimbia makazi yao kaskazini mwa Msumbiji ndani ya wiki mbili pekee. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya Jumanne ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, ambalo limeonya juu ya mashambulizi kuongezeka na kuyakumba maeneo ambayo hapo awali yalikuwa salama, na hivyo kuongeza mzigo wa wahudumu wa kibinadamu waliokwisha elemewa.
-
Wakuu wa ECOWAS wazuru Guinea-Bissau baada ya mapinduzi ya kijeshi
Dec 02, 2025 23:08Ujumbe wa upatanishi wa ngazi ya juu kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ulifanya mkutano Jumatatu na viongozi wa mpito wa Guinea-Bissau kujadili njia ya amani ya kumaliza mgogoro wa kisiasa uliosababishwa na mapinduzi ya kijeshi ya wiki iliyopita.
-
Rais Samia: Vurugu za uchaguzi zililenga kuiangusha serikali
Dec 02, 2025 09:54Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefichua kuwa vurugu za uchaguzi wa Oktoba 29 ziliratibiwa na watu wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuibomoa serikali, na kuzionya vikali taasisi za dini.
-
Sakata la usalama, Waziri wa Ulinzi wa Nigeria ajiuzulu
Dec 02, 2025 09:50Waziri wa Ulinzi wa Nigeria, Mohammed Badaru Abubakar amejiuzulu, katika kipindi ambacho nchi hiyo inakabiliwa na mgogoro wa usalama unaojumuisha utekaji nyara wa watoto wa shule kwa wingi.
-
Viongozi wa Afrika watoa wito wa kutambuliwa rasmi uhalifu wa enzi za ukoloni na kulipwa fidia
Dec 02, 2025 02:55Viongozi wa Afrika waliokutana Algiers siku ya Jumapili walitoa wito wa kutambuliwa rasmi uhalifu uliofanyika enzi za ukoloni barani Afrika, ufanywe kuwa ni uhalifu na kulipwe fidia kupitia mchakato unaoungwa mkono na Umoja wa Afrika.