-
Jeshi la Sudan lakabiliana na mashambulizi ya droni katika mji mkuu Khartoum
Nov 08, 2025 00:38Jeshi la Sudan limetangaza kuwa kikosi chake cha ulinzi wa anga jana Ijumaa kilinasa kundi la ndege zisizo na rubani (droni) zilizokusudia kufanya mashambulizi katika mji wa Omdurman, magharibi mwa Khartoum, na katika mji wa kaskazini wa Atbara.
-
Watu 145 washtakiwa kwa uhaini wakidaiwa kuhusika katika maandamano ya vurugu Tanzania
Nov 08, 2025 00:37Waendesha mashtaka nchini Tanzania jana Ijumaa wamewashtaki takriban watu 145 kwa kosa la uhaini madai ya kuhusika katika maandamano ya vurugu yaliyozuka wakati wa uchaguzi wa rais na bunge wiki iliyopita.kulingana na faili za mahakama zilizoonekana na Reuters.
-
Kenya yataka majibu kwa Tanzania kuhusu raia wake waliokumbwa na misukosuko ya baada ya uchaguzi
Nov 07, 2025 08:21Kenya imeitaka Tanzania itoe majibu kuhusu hali ya raia wake waliojipata kwenye mzozo wa baada ya uchaguzi, huku ikishinikiza serikali ya nchi hiyo ihakikishe usalama wao na kuchukua hatua dhidi ya ukiukaji wa haki zao.
-
Rais mzee zaidi duniani aapishwa kuongoza Cameroon kwa muhula wa nane
Nov 07, 2025 03:52Kiongozi wa muda mrefu wa Cameroon, Paul Biya, ameapishwa kwa muhula mpya wa miaka saba kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa rais wa mwezi uliopita, ambao mpinzani wake ameutaja kama "mapinduzi ya kikatiba".
-
Wanamgambo wa RSF waafiki pendekezo la kusitisha vita Sudan
Nov 07, 2025 03:38Vikosi vya Usaidizi wa Haraka vya Sudan (RSF) vimetangaza kwamba vinakubali usitishaji vita uliopendekezwa na Kamati ya Kimataifa ya Pande Nne.
-
Rwanda yashutumu ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa mafunzo ya jeshi la DRC
Nov 07, 2025 00:15Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Rwanda, amekosoa ujumbe wa kueneza amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) kwa kutoa mafunzo kwa wanajeshi 120 wa DRC.
-
Afrika Kusini yachunguza madai ya raia wake kupigana kama mamluki kwenye vita vya Ukraine
Nov 06, 2025 23:05Afrika Kusini imesema kuwa, raia wake 17 waliojiunga na makundi ya mamluki katika vita vya Russia na Ukraine wameomba msaada wa kuokolewa kutoka kwenye eneo la Donbas ambako mapigano yanaendelea.
-
Zaidi ya watu 30 wapoteza maisha katika mafuriko nchini Sudan
Nov 06, 2025 23:03Mafuriko makubwa yamelikumba Jimbo la Nile nchini Sudan na kupelekea zaidi ya watu 30 kupoteza maisha na maelfu ya wengine kukwama kutokana na nyumba na maeneo yao kujaa maji ya mafuriko.
-
Waangalizi wa AU: Uchaguzi wa Tanzania haukukidhi viwango vya kimataifa
Nov 06, 2025 07:42Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Afrika katika uchaguzi mkuu wa wiki iliyopita nchini Tanzania uliogubikwa na ghasia umeeleza kuwa uchaguzi huo haukukidhi viwango vya kimataifa vya kidemokrasia.
-
EU yataka kufunguliwa korido ya kibinadamu mashariki mwa Kongo
Nov 06, 2025 07:39Afisa wa Umoja wa Ulaya ametoa wito kwa pande husika katika mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufungua koridi ya kibinadamu na kuruhusu kuanza kuingia kwa ndege za misaada ya kibinadamu.