-
Uchaguzi wa urais Kenya ukifanyika leo Ruto atashinda, lakini utaingia katika duru ya pili
Dec 28, 2025 23:50Utafiti uliofanywa na kampuni ya Infotrak unaonyesha kuwa, endapo uchaguzi wa urais wa Kenya ungefanyika hivi leo, Rais William Ruto angeibuka mshindi; hata hivyo uchaguzi huo ungelazimu kuingia katika duru ya pili kwa sababu ushindi wake usingevuka kiwango cha asilimia 50+1 ya kura kinachohitajika.
-
Vikwazo vya UK vyazilazimisha Angola na Namibia zikubali kupokea wahamiaji wanaorejeshwa
Dec 28, 2025 23:50Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza imetangaza kuwa, Angola na Namibia zimekubali kuruhusu kurejeshwa katika nchi hizo wahamiaji wasio rasmi na wahalifu baada ya serikali ya Uingereza kutishia kutoa adhabu ya vikwazo vya viza kwa nchi zinazokataa kutoa ushirikiano.
-
Baraza la Usalama na Arab League kukutana kujadili hatua ya Israel ya kuitambua rasmi Somaliland
Dec 28, 2025 08:07Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) zimepanga kufanya mikutano tofauti wiki hii kujadili matokeo ya hatua ya Israel ya kulitambua rasmi eneo la 'Somaliland, ambalo limejitenga na Somalia, kama taifa huru na lenye mamlaka kamili.
-
Wanawake na watoto ni kati watu zaidi ya 200 waliouawa katika mauaji mapya ya kikabila huko Darfur
Dec 28, 2025 07:09Mtandao wa Madaktari wa Sudan umeripoti kuwa watu zaidi ya 200, wakiwemo wanawake na watoto wameuawa katika mashambulizi ya kikabila yaliyofanywa na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) huko Darfur nchini Sudan.
-
Jamhuri ya Afrika ya Kati yaendesha uchaguzi mkuu,Touadéra anawania muhula wa tatu wa urais
Dec 28, 2025 06:52Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wameelekea kwenye masanduku ya kura katika zoezi la uchaguzi mkuu huku Rais Archange Touadéra akiwania kiti cha urais kwa muhula wa tatu.
-
Somalia yaitaka Israel ifute uamuzi wake wa kuitambua Somaliland
Dec 27, 2025 23:23Somalia imeitaka Israel kubatilisha hatua yake ya kulitambua rasmi eneo la 'Somaliland, ambalo limejitenga na Somalia, kama taifa huru na lenye mamlaka kamili. Somalia imelaani hatua hiyo na kuitaja kuwa kitendo cha "uchokozi ambacho kamwe hakitavumiliwa.
-
Guinea Conakry kufanya uchaguzi wa urais wa kihistoria leo Jumapili; Mamadi Doumbouya anashiriki
Dec 27, 2025 23:22Guinea Conakry leo Jumapili inatarajiwa kufanya uchaguzi wake wa kwanza wa urais tangu baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 2021. Zoezi hili linayoashiria hatua muhimu katika kipindi cha uongozi wa mpito wa nchi hiyo kuelekea katika utawala wa kikatiba.
-
Ujumbe wa kwanza wa Umoja wa Mataifa wawasili El Fasher kutathmini hali ya mambo
Dec 27, 2025 07:46Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema shirika hilo limefanikiwa kupeleka ujumbe wa tathmini huko El Fasher, mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan.
-
Israel yalaaniwa vikali kwa kutambua Somaliland kama nchi huru
Dec 27, 2025 03:11Utawala wa Kizayuni wa Israel umetangaza kutambua eneo la 'Somaliland, ambalo limejitenga na Somalia, kama taifa huru na lenye mamlaka kamili.
-
Wataalamu: Operesheni ya kijeshi ya Marekani nchini Nigeria inalenga kugawa taifa
Dec 27, 2025 03:10Wataalamu wametilia shaka lengo la Rais wa Marekani, Donald Trump, katika mashambulizi ya kijeshi nchini Nigeria kwa kisingizio cha kupambana na magaidi wa kundi la DAESH (ISIS/ISIL) kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.