-
Mapitio ya jinai za Magharibi; jinai za Marekani nchini Somalia
Nov 04, 2025 23:06Marekani imefanya mashambulizi ya anga na operesheni za kijeshi nchini Somalia, na kusababisha vifo vingi vya raia, na akthari ya hatua hizo zimekuwa zikikosolewa na makundi ya kutetea haki za binadamu. Idadi halisi ya vifo inaweza kuwa kubwa zaidi kuliko ile iliyotangazwa na Pentagon.
-
Guterres: Uhalifu wa kivita nchini Sudan hauwezi kupita hivihivi bila kuadhibiwa
Nov 04, 2025 07:47Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kusimamisha mapigano nchini Sudan, akisisitiza kwamba moja ya masharti muhimu ya kukomesha vita ni kuzuia silaha mpya kuingia nchini humo, na kusisitiza kwamba kuendelea mtiririko wa silaha kunarefusha mzozo na kuzidisha mateso ya raia.
-
Kwa uchache watu 20 wameuawa katika mashambulizi ya droni ya RSF nchini Sudan
Nov 04, 2025 03:28Watu wasiopungua 20 wameuawa na wengine 34 kujeruhiwa jana Jumatatu katika mashambulizi mawili tofauti ya droni na ndege zisizo na rubani na Vikosi cha Usaidizi wa Haraka cha Kijeshi (RSF) huko katikati na magharibi mwa Sudan.
-
Mahakama ya ICC: Matukio ya El-Fasher yanaweza kuainishwa kama uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu
Nov 03, 2025 22:53Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetoa tamko juu ya wasiwasi mkubwa uliozuka kufuatia ripoti mpya kutoka El-Fasher, jimboni Darfur Kaskazini, nchini Sudan, zikielezea kufanyika mauaji ya halaiki, ubakaji, na uhalifu mwingine unaodaiwa kufanywa wakati wa mashambulizi ya Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF).
-
Mama Samia aapishwa kwa muhula mwingine wa urais
Nov 03, 2025 08:05Dkt. Samia Suluhu Hassan wa Tanzania ameapishwa leo Jumatatu kuiongoza nchi hiyo kwa muhula mpya wa miaka mitano. Rais Samia ameapishwa baada ya uchaguzi uliogubikwa na vurugu.
-
Mapigano ya jeshi na wanamgambo RSF yaendelea huku walimwengu wakishindwa kuzipatanisha pande hasimu
Nov 03, 2025 06:38Vita haribu na angamizi vya Sudan viinaendelea huku jamii ya kimataifa ikioonekana kushindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro huo wa ndani.
-
Jeshi la Uganda lazima mashambulizi ya waasi magharibi mwa nchi
Nov 03, 2025 03:03Jeshi la Uganda UPDF limetangaza kuwa, limefanikiwa kuzima mlolongo wa mashambulizi yaliyoratibiwa vyema na vikundi vyenye silaha ambavyo vilishambulia vituo vya kijeshi na polisi katika maeneo ya magharibi ya nchi hiyo.
-
Rais Tshisekedi: Mazungumzo ya amani na waasi wa M23 yataanza tena Doha
Nov 03, 2025 03:02Rais Felix Tshisekedi wa DRC amesema kuwa, mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kundi la waasi la Machi 23 (M23) yataanza tena wiki ijayo huko Doha, mji mkuu wa Qatar.
-
Wasudan 177,000 wamekwama katika mji ulioteketea
Nov 02, 2025 22:53Mji wa El Fasher, ambao ni makao makuu ya jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan, hatimaye ulitekwa na Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF hivi karibuni baada ya kuzingirwa kwa muda wa miezi 18 na hivi sasa ripoti zinasema kuwa Wasudan 177,000 wamekwama kwenye mji huo.
-
Wahamiaji 45 wasio na vibali waokolewa pwani ya mashariki ya Libya
Nov 02, 2025 22:51Wahamiaji 45 wasio na vibali wameokolewa kwenye pwani ya mji wa Tobruk wa mashariki mwa Libya. Hayo ni kwa mujibu wa gazeti la Libya Al-Watan ambalo limesema kuwa wahamiaji hao wamekabidhiwa kwa mamlaka husika baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.