-
Viongozi wa upinzani Kenya wasema wana hofu ya kuenea machafuko ya kisiasa na kuhatarisha uchaguzi wa 2027
Sep 15, 2026 03:58Viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani nchini Kenya wameonya kuwa ghasia za kisiasa zinaweza kuenea na kuhatarisha uchaguzi mkuu wa 2027.
-
Libya yakamata dawa za kulevya za picha ya Gaddafi zilizoingizwa kutokea Ulaya
Sep 14, 2026 11:32Libya imekamata shehena ya maelfu ya vidonge vya dawa za kulevya aina ya ecstasy, vilivyowekwa alama ya picha ya kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi.
-
Mlipuko wa ugonjwa wa Kimeta (Anthrax) waua wanyamapori nchini Zambia na kuwaambukiza binadamu
Sep 14, 2026 09:28Mlipuko wa ugonjwa wa kimeta (anthrax) katika eneo la kaskazini mwa Zambia umesababisha vifo vya viboko 46, tembo wanane, nyati watano na mamba mmoja, huku watu 12 wakiripotiwa kuambukizwa ugonjwa huo baada ya kula nyama ya wanyama hao waliokufa ambao walikutwa na vimelea vya ugonjwa huo, kulingana na mamlaka husika.
-
Afrika Kusini yatoa mwito kwa BRICS kutetea ushirikiano wa pande nyingi
Sep 14, 2026 07:32Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametoa mwito kwa nchi za BRICS kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi na kushinikiza mageuzi ya mfumo wa kimataifa akisema kuwa sauti za Afrika na nchi za kusini mwa dunia lazima zisikike kikamilifu kimataifa.
-
Maimamu sita wa Nigeria watekiwa wakiwa njiani kwenda kuombea kuchaguliwa upya kwa Rais
Sep 13, 2026 11:53Watu wenye silaha wamewateka nyara maimamu sita nchini Nigeria kaskazini mwa nchi hiyo, Polisi wametangaza leo Jumapili.
-
Mlipuko wa Ebola DRC wavuka kiwango cha wagonjwa 7,000 na kuenea hadi mkoa wa saba
Sep 13, 2026 07:18Ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) umevuka kiwango cha wagonjwa 7,000 waliothibitishwa na kufikia mkoa wa saba baada ya mgonjwa wa kwanza kugundulika katika mkoa wa Sud-Ubangi.
-
Niger yateua mkuu mpya wa majeshi baada ya jaribio la uasi lililozimwa
Sep 13, 2026 07:13Serikali ya kijeshi ya Niger imemteua mkuu mpya wa jeshi, kufuatia jaribio la uasi wa jeshi lililozimwa mwezi uliopita. Hayo ni kwa mujibu taarifa iliyotolewa na televisheni ya taifa.
-
Siku ya kuzaliwa Rais wa Zimbabwe yatangazwa Sikukuu ya Kitaifa, itaitwa Siku ya Munhumutapa
Sep 13, 2026 07:00Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza Septemba 15, siku yake ya kuzaliwa, kuwa sikukuu mpya ya umma. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la serikali la Herald.
-
AU yaadhimisha miaka 24 kwa mwito wa umoja wa bara zima na ushawishi wa kimataifa
Sep 11, 2026 09:24Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), Mahmoud Ali Youssouf, ametoa mwito wa kujitolea zaidi kwa kuzingatia misingi ya Umoja wa Waafrika (Pan-Africanism), mshikamano na umoja wa bara hilo zima. Ametoa mwito huo katika maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Afrika (AU).
-
Vyombo vya kutunga sheria vya Libya vyasisitiza mchakato wa kisiasa ufuate Katiba
Sep 11, 2026 09:20Vyombo viwili vikuu vya nchini Libya yaani Baraza la Wawakilishi la Libya (HoR) na Baraza Kuu la Serikali (High Council of State) vimesisitiza kuwa mchakato wa kisiasa wa nchi hiyo unapaswa kufanyika ndani ya mfumo wa Tamko la Katiba na Makubaliano ya Kisiasa yanayosimamia kazi za mabaraza hayo mawili.