-
Algeria yakata uhusiano wake wa kidiplomasia na Umoja wa Falme za Kiarabu
Sep 11, 2026 04:28Algeria imekata uhusiano wake wa kidiplomasia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) baada ya miaka kadhaa ya kuongezeka kwa mvutano kati ya nchi hizo mbili.
-
Vifo vya ugonjwa wa difteria katika Jimbo la Plateau nchini Nigeria vyafikia 27
Sep 11, 2026 04:11Idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa difteria (diphtheria) katika Jimbo la Plateau katikati ya Nigeria imepanda hadi 27, huku idadi ya visa vinavyoshukiwa ikiongezeka maradufu na kufikia 303, mamlaka za afya zilisema Jumatano.
-
WFP: Maeneo yenye Ebola DRC sasa yanakumbwa na njaa
Sep 11, 2026 04:10Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mapambano dhidi ya mlipuko wa sasa wa Ebola huko mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu, hayawezi kutenganishwa na juhudi za kuhakikisha wananchi wanapata chakula cha kutosha.
-
Mufti wa Tanzania awataka Waislamu wafunge siku 3 kuomba El Nino iwe ya rehma, isiwe ya adhabu
Sep 10, 2026 02:49Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally, ametoa wito kwa Mashekhe na Waislamu kwa ujumla kufunga kwa siku tatu kuanzia leo Alkhamisi Septemba 10, 2026, huku akiwataka wamuombe Mwenyezi Mungu aliepushe taifa na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa zinazotabiriwa.
-
WHO: Vituo vya Ebola Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimezidiwa
Sep 10, 2026 02:47Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, vituo vya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimeelemewa kutokana na kuongezeka idadi ya maambukizi ya ugonjwa huuo.
-
Mgomo wa wauguzi Kenya waendelea kusababisha maafa, makumi ya wagonjwa wafariki mahospitalini
Sep 09, 2026 10:20Wagonjwa wanawake wapatao 22 wameaga dunia kutokana na matatizo yanayohusiana na uzazi katika kipindi cha wiki moja katika hospitali za Kenya huku mgomo wa wauguzi ukiwa unaendelea.
-
Moto uliozuka kwenye msitu wa Mlima Kenya umeteketeza ekari 30,000 za maeneo ya nyanda za juu
Sep 09, 2026 03:07Ekari zipatazo 30,000 za maeneo ya nyanda za juu katika Msitu wa Mlima Kenya zimeteketea kutokana na moto mkali uliozuka mwanzoni mwa mwezi huu.
-
MSF: Wahamiaji zaidi ya elfu moja wanaotokea Gambia wameokolewa katika pwani ya Afrika Magharibi
Sep 09, 2026 03:05Shirika la Misaada la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limetangaza kuwa, wahamiaji zaidi ya 1,000 wameokolewa katika kipindi cha wiki moja kwenye pwani ya Afrika Magharibi wakati wakijaribu kuvuka bahari hatari kuelekea Ulaya.
-
Msaada wa kigeni kwa RSF ndio sababu kuu ya kuendelea kwa vita nchini Sudan
Sep 08, 2026 11:17Msaada wa nje kwa kundi la waasi la Rapid Support Forces (RSF) ndiyo sababu kuu ya kuendelea kwa vita vya muda mrefu na jinai nchini Sudan. Hayo yamedokezwa na mwanasheria mkuu wa nchi hiyo siku ya Jumatatu, akitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti za kukomesha hali hiyo.
-
Kongo yaimarisha udhibiti wa serikali kwa data za uchimbaji madini
Sep 08, 2026 11:00Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza kuwa inaratibu mpango wa kuimarisha udhibiti wa serikali kwa data ya kijiolojia ili kuboresha mapato ya mabilioni ya dola katika sekta ya uchimbaji madini kwa lengo la kusimamia pakubwa maendeleo ya utajiri mkubwa wa madini wa nchi hiyo.