-
Watu wa Afrika walaani jinai za utawala wa Israel dhidi ya Yemen na Gaza
Sep 05, 2025 06:54Wananchi wa nchi kadhaa za Afrika wamefanya maandamano makubwa kulaani jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Yemen na Gaza, wakionesha mshikamano wa wazi na harakati za ukombozi wa Wapalestina.
-
Afrika CDC: Mpox bado ni dharura ya kiafya barani Afrika
Sep 05, 2025 03:34Ugonjwa wa Mpox ambao umeenea katika nchi za Kiafrika na kuua mamia ya watu, bado ni dharura ya kiafya katika bara hilo. Taarifa hii imetolewa na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Barani Afrika (Africa CDC).
-
Mjukuu wa Mandela: Mateso ya Waafrika Kusini weusi chini ya apartheid si lolote ikilinganishwa na masaibu ya Wapalestina
Sep 05, 2025 00:20Mjukuu wa kiongozi wa mapambano ya ukombozi wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela, Mandla Mandela, amelaani mzingiro wa utawala wa Israel na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo dhidi ya watu wa Palestina, akisema kwamba mateso yanayowapata Wapalestina chini ya utawala vamizi wa Israel ni mabaya zaidi kuliko yale yaliyowapata Waafrika Kusini weusi chini ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
-
Njaa yaongezeka nchini Nigeria sambamba na kupungua usambazaji wa chakula
Sep 04, 2025 22:53Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema watu milioni 31 wanakabiliwa na uhaba wa chakula nchini Nigeria, hasa kaskazini mashariki, ambako watu milioni 2.3 wamelazimika kuacha makazi na mashamba yao katika kipindi cha miaka 15 ya vita.
-
Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Zambia ahukumiwa kifungo cha miaka 4 jela kwa ufisadi
Sep 04, 2025 09:44Mahakama ya Zambia leo Alhamisi imemhukumu Joseph Malanji aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kifungo cha miaka minne jela na kazi ngumu kwa kupatikana na hatia ya ufisadi.
-
Ajali nyingine ya boti yaua watu zaidi ya 60 nchini Nigeria
Sep 04, 2025 04:13Kwa akali watu 60 wamefariki dunia baada ya mashua iliyokuwa imebeba zaidi ya abiria 100 kupinduka na kuzama katika jimbo la Niger, kaskazini mwa Nigeria.
-
Tunisia yaijia juu polisi ya Ufaransa kwa kuua raia wake Marseille
Sep 04, 2025 04:06Tunisia imewasilisha malalamiko rasmi kwa Ufaransa, ikilaani mauaji ya raia wa nchi hiyo ya Kiarabu yaliyofanywa na polisi wa Ufaransa katika mji wa kusini wa Marseille.
-
Serikali ya DRC: Mwanamfalme wa Qatar atawekeza dola bilioni 21 katika sekta kadhaa
Sep 03, 2025 23:43Serikali ya Jamhuri ya Kidemokorasia ya Kongo, DRC kupitia ofisi ya Waziri Mkuu wake imetangaza kuwa, Mwanamfalme wa Qatar Sheikh Mansour bin Jabir bin Jassim Al Thani anataka kuwekeza nchini humo dola bilioni 21 katika sekta mbalimbali zikiwemo za kilimo na uchimbaji madini.
-
Misri kutuma vikosi vya kulinda amani Somalia huku Ethiopia ikionyesha wasiwasi
Sep 03, 2025 09:51Misri inapanga kutuma kikosi cha kulinda amani nchini Somalia chini ya Mpango wa Msaada wa Umoja wa Afrika kwa Somalia (AUSSOM). Ingawa Ethiopia haijatoa kauli ya wazi, lakini huko nyuma ilibainisha kutoafiki ushiriki wa wanajeshi wa Misri katika kikosi hicho cha Umoja wa Afrika.
-
DRC yatuhumu waasi wa M23 kwa ukiukaji wa haki za binadamu, kujumuisha vijana kwa nguvu vitani
Sep 03, 2025 09:25Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewatuhumu waasi wa M23 kwa ukiukaji wa haki za binadamu na kuwalazimisha vijana kujiunga na harakati za kijeshi mashariki mwa nchi.