-
AU yataka mahasimu Sudan kusitisha vita ili kutoa fursa ya ufikishaji misaada baada ya maporomoko ya ardhi
Sep 02, 2025 23:03Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mohamoud Ali Youssuf, amezitaka pande zinazozozana nchini Sudan kusitisha mapigani ili kuruhusu utoaji wa haraka wa misaada ya kibinadamu kufuatia maporomoko ya ardhi.
-
Burkina Faso yapitisha sheria inayoharamisha na kujinaisha mapenzi ya jinsia moja
Sep 02, 2025 07:48Kikosi tawala cha kijeshi cha Burkina Faso kimepitisha sheria inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja na kutangaza adhabu ya kifungo cha hadi miaka mitano jela kwa watu wote watakaopatikana na hatia ya kujihusisha na vitendo hivyo vichafu. Wageni watakaopatikana na hatia pia watafukuzwa nchini humo kwa mujibu wa sheria hiyo mpya.
-
Ulimaji viazi ulivyobadili sekta ya kilimo nchini Lesotho
Sep 02, 2025 07:40Ulimaji viazi nchini Lesotho kusini mwa bara la Afrika unapewa kipaumbele na umekuwa ishara kuu ya mabadiliko katika sekta ya kilimo ya nchi hiyo baada ya kuonekana kama chakula kikuu cha familia.
-
Zaidi ya 1,000 waaga dunia katika maporomoko ya ardhi Darfur, Sudan
Sep 02, 2025 03:33Kwa akali watu 1,000 wamepoteza maisha katika maporomoko ya ardhi yaliyoharibu kijiji kizima katika eneo la Milima ya Marra magharibi mwa Sudan.
-
AU yatiwa wasiwasi na makubaliano ya mataifa ya Afrika kupokea wahamiaji wa Marekani
Sep 02, 2025 02:56Baraza la haki la Umoja wa Afrika (AU) limeelezea wasiwasi wake kuhusu makubaliano ya Washington na nchi kadhaa za Afrika, ambayo yanaruhusu nchi hizo za Kiafrika kupokea wahamiaji waliofukuzwa Marekani.
-
Zaidi ya visa 100,000 vya kipindupindu vimeripotiwa Sudan huku njaa ikishadidi
Sep 01, 2025 22:50Zaidi ya maambukizi 100,000 ya kipindupindu yameripotiwa katika nchi ya Sudan iliyokumbwa na vita katika mwaka mmoja, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA) ilisema Jumatatu.
-
Umoja wa Afrika waguswa na kuongezeka kwa fedha haramu barani Afrika
Sep 01, 2025 07:42Umoja wa Afrika, umeeleza kuguswa na kuongezeka kwa fedha haramu kwenye bara hilo.
-
Marufuku ya kutotoka nje yawekwa maeneo yenye ghasia za kikabila Kenya
Sep 01, 2025 07:34Serikali ya Kenya imetangaza kuweka marufuku ya kutotoka nje katika maeneo yenye ghasia za kikabila katika nchi hiyo ya Afrika Mashaariki.
-
Kamanda wa wanamgambo wa RSF aapishwa kuwa Mkuu wa serikali sambamba huko Sudan
Sep 01, 2025 04:15Mohammed Hamdan Dagalo kamanda wa wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) jana aliapishwa kuwa kiongozi wa serikali sambamba nchini Sudan.
-
Wasiwasi wa UN kuhusu kuongezeka wapiganaji karibu na mji mkuu wa Libya
Aug 31, 2025 08:49Ofisi ya Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) imeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa wapiganaji wenye silaha nzito karibu na mji mkuu Tripoli, ikionya kuwa “matukio hatari” yanaweza “kuleta madhara” kwa raia.