Maelfu waandamana Afrika Kusini wakitaka kukatwa uhusiano wa nchi hiyo na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i131334-maelfu_waandamana_afrika_kusini_wakitaka_kukatwa_uhusiano_wa_nchi_hiyo_na_israel
Watu zaidi ya elfu tatu jana waliandamana katika mji wa Cape Town Afrika Kusini wakiitaka nchi hiyo kukata uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na Israel, ikiwa ni pamoja na kufunga ubalozi wake kufuatia vita na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala huo katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2025-09-28T07:01:41+00:00 )
Sep 28, 2025 07:01 UTC
  • Maelfu waandamana Afrika Kusini wakitaka kukatwa uhusiano wa nchi hiyo na Israel

Watu zaidi ya elfu tatu jana waliandamana katika mji wa Cape Town Afrika Kusini wakiitaka nchi hiyo kukata uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na Israel, ikiwa ni pamoja na kufunga ubalozi wake kufuatia vita na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala huo katika Ukanda wa Gaza.

Serikali ya Afrika Kusini imekuwa ikikosoa pakubwa jinai za Israel huko Gaza,ambapo mwezi Disemba mwaka juzi  iliwasilisha kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ikivitaja vita vya Israel katika Ukanda wa Gaza kuwa sawa na mauaji ya kimbari shtaka ambalo Israel imelikanusha.

Maandamano ya jana huko Cape Town, Afrika Kusini yalizikutanisha pamoja taasisi kadhaa zinazoiunga mkono Palestina, vyama vya kisiasa na makundi ya Waislamu na Wakristo. Maandamano hayo yametajwa kuwa moja kati ya maandamano makubwa kuwahi kushuhudiwa nchini Afrika Kusini katika miezi ya karibuni. 

Usuf Chikte Mratibu wa Kampeni ya Mshikamano na Palestina amesema kuwa Afrika Kusini inapasa kuisusia na kuiwekea vikwazo Israel sawa kabisa na hatua zilizochukuliwa kimataifa kuushinikiza utawala wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini. 

Mratibu huyo wa Kampeni ya Mshikamano na Palestina aliuambia umati wa watu walioandamana kwamba serikali inapasa kuchukua hatua ya "kumfukuza balozi na kuufunga ubalozi wa Israel nchini Afrika Kusini  na kutengwa utawala huo na mashirika ya kimataifa ya michezo kama vile FIFA.