-
Afrika Kusini yatangaza janga la kitaifa kufuatia mvua na mafuriko yaliyouwa watu 30
Jan 19, 2026 11:35Afrika Kusini imetangaza janga la kitaifa kutokana na mvua kubwa na mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya takriban watu 30 kaskazini mwa nchi hiyo, kuharibu maelfu ya nyumba na kusomba barabara na madaraja.
-
Mafuriko yasababisha vifo vya watu 10 Afrika Kusini, na kusababisha kufungwa Hifadhi ya Kruger
Jan 16, 2026 07:14Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa kaskazini-mashariki mwa Afrika Kusini yamesababisha vifo vya watu 10 kwa usiku mmoja na kupelekea kufungwa kwa Hifadhi ya Taifa ya Kruger.
-
ANC yaonya kuhusu njama za 'mapinduzi' nchini Iran
Jan 16, 2026 02:13Mkuu wa vuguvugu la Mshikamano wa Kimataifa wa chama tawala cha African National Congress (ANC) katika jimbo la Western Cape nchini Afrika Kusini ameonya kwamba, machafuko ya hivi karibuni nchini Iran yana mkono wa Marekani na washirika wake wa Kizayuni.
-
Afrika Kusini: Hatutazuia mpango wa Washington wa kuwapa hifadhi wazungu waliowachache
Jan 08, 2026 13:03Afrika Kusini imesema haitapinga mpango wenye utata wa serikali ya Washington wa kuwapeleka Marekani raia wazungu walio wachache wa Afrika Kusini.
-
Afrika Kusini yataka UN iitishe kikao cha dharura kufuatia mashambulizi ya Marekani dhidi ya Venezuela
Jan 04, 2026 03:01Afrika Kusini imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitisha kikao cha dharura kufuatia mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela, na kukamatwa Rais wa nchi hiyo Nicholas Maduro na mkewe.
-
Kisu cha ngariba; Vijana 41 waaga dunia Afrika Kusini wakipashwa tohara
Dec 31, 2025 10:17Takriban vijana 41 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na taratibu 'zisizofaa' za upashaji tohara nchini Afrika Kusini mwezi Novemba na Desemba mwaka huu unaomalizika wa 2025, mamlaka za nchi hiyo zilitangaza hayo jana Jumanne.
-
Makundi ya kiraia A/Kusini yataka kupewa dhamana wanaharakati wa Palestina waliogoma kula katika jela za UK
Dec 23, 2025 08:08Makundi kadhaa ya kiraia nchini Afrika Kusini yametoa wito yakitaka kupewa dhamana haraka iwezekanavyo wanaharakati wawili watetezi wa Palestina waliogoma kula katika jela za Uingereza yakisema kuwa kuendelea kufungwa raia hao kunahatarisha maisha yao.
-
Ufyatuaji risasi Afrika Kusini; watu wenye silaha waua 9 karibu na Johannesburg
Dec 21, 2025 07:43Watu waliokuwa na silaha, usiku wa kuamkia leo, wamefyatua risasi kiholela katika kitongoji kimoja karibu na Johannesburg nchini Afrika Kusini na kuua takriban watu 9 na kujeruhi wengine kadhaa.
-
Rais wa Afrika Kusini amtuhumu Trump kwa kutoa 'kauli zisizo za kweli' kuhusu nchi yake
Dec 01, 2025 03:07Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini jana alimtuhumu Rais Donald Trump wa Marekani kwa kuendelea kutoa "taarifa zisizo za kweli" kuhusu nchi yake.
-
Kwa nini Macron anaamini kuwa G20 inakaribia kuporomoka?
Nov 24, 2025 07:54Katika ufunguzi wa mkutano wa kilele wa G20 mjini Johannesburg, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alisema katika hotuba isiyo ya kawaida kuwa kundi hilo limepoteza uwezo wake wa kutatua migogoro ya kimataifa.