-
Video inayowaonesha wanajeshi wa SEPAH wa Iran wakiionya manuwari ya kivita vya Uingereza isiingilie operesheni ya kuzuia meli ya mafuta ya nchi hiyo
Jul 29, 2019 16:18Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH limesambaza mkanda wa video na sauti wakati jeshi hilo lilipotoa onyo kwa Manuwari ya Kifalme wa Uingereza kwamba ikae mbali na isiingilie operesheni ya kusimamishwa meli ya mafuta iliyokuwa inapeperushwa bendera ya Uingereza katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
-
Kikao cha dharura cha kamisheni ya pamoja ya JCPOA mjini Vienna; matarajio ya fursa ya mwisho iliyobakia ya kuokoa JCPOA
Jul 29, 2019 03:35Kikao cha dharura cha kamisheni ya pamoja ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kilifanyika jana Jumapili huko Vienna Austria kwa ombi la Ufaransa, Uingereza, Ujerumani na Iran kwa kuhudhuriwa na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kwa uongozi wa Sayyid Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na Helga Maria Schmid, Naibu Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya.
-
Mousavi: Iran inasubiri hatua za kivitendo za Ulaya katika kulinda makubaliano ya JCPOA
Jul 29, 2019 09:32Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inasubiri kuona hatua za kivitendo za nchi za Ulaya katika kulinda makubaliano ya nyuklia maarufu kwa kifupi kwa jina la JCPOA.
-
Spika Larijani: Mkakati wa Iran ni kuinua kiwango cha usalama Mashariki ya Kati
Jul 28, 2019 23:52Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya stratijia ya Tehran ya kuinua kiwango cha usalama katika Mashariki ya Kati na kusema kwamba, usalama wa eneo hili unaweza kuletwa na nchi husika za eneo hili na si vinginevyo.
-
Araqchi: Kikao cha kamisheni ya JCPOA kimekuwa na mafanikio
Jul 28, 2019 23:52Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa kikao cha kamisheni ya pamoja ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kilichofanyika jana mjini Vienna kimemalizika kwa mafanikio japo hatuwezi kusema kuwa mambo yote yametatuliwa.
-
Kikao cha kamisheni ya pamoja ya JCPOA chaanza kufanyika Vienna, Austria
Jul 28, 2019 07:53Kikao cha kamisheni ya pamoja ya makubaliano ya nyuklia JCPOA cha Manaibu Mawaziri na Wakurugenzi wa Kisiasa wa Iran na kundi la 4+1 pamoja na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kimeanza leo huko Vienna mji mkuu wa Austria.
-
Rais Rouhani: Uwepo wa vikosi vya kigeni ndio chimbuko kuu la mizozo Mashariki ya Kati
Jul 28, 2019 07:54Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, vikosi vya kigeni si tu kwamba, havisaidii chochote kwa usalama wa Mashariki ya Kati bali ni chanzo kikuu cha mizozo na migogoro katika eneo hili.
-
Mashauriano kuhusu matukio ya eneo; lengo la mazungumzo ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Oman
Jul 27, 2019 23:40Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Oman jana Jumamosi walikutana hapa mjini Tehran kwa lengo la kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu matukio muhimu ya kieneo na kimataifa.
-
Ali Shamkhani: Nchi zote zinapaswa kuheshimu sheria za kimataifa za baharini
Jul 27, 2019 23:38Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa, mataifa yote ya dunia yanapaswa kuheshimu sheria za kimataifa za baharini kwa ajili ya kulinda usalama na kwamba, Iran haina ubaguzi baina ya nchi na nchi kuhusiana na suala hilo.
-
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Oman zasisitiza kuimarisha ushirikiano baina yao
Jul 27, 2019 09:45Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Oman leo wamekutana hapa mjini Tehran ambapo pamoja na mambo mengine wamesisitiza juu ya kuimarisha ushirikiano wa pande mbili.