Ali Shamkhani: Nchi zote zinapaswa kuheshimu sheria za kimataifa za baharini
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55033-ali_shamkhani_nchi_zote_zinapaswa_kuheshimu_sheria_za_kimataifa_za_baharini
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa, mataifa yote ya dunia yanapaswa kuheshimu sheria za kimataifa za baharini kwa ajili ya kulinda usalama na kwamba, Iran haina ubaguzi baina ya nchi na nchi kuhusiana na suala hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 27, 2019 23:38 UTC
  • Ali Shamkhani: Nchi zote zinapaswa kuheshimu sheria za kimataifa za baharini

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa, mataifa yote ya dunia yanapaswa kuheshimu sheria za kimataifa za baharini kwa ajili ya kulinda usalama na kwamba, Iran haina ubaguzi baina ya nchi na nchi kuhusiana na suala hilo.

Ali Shamkhani alisema hayo jana katika mazungumzo yake hapa mjini Tehran na Yusuf bin Alawi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Oman ambapo alisisitiza pia udharura wa kupanuliwa ushirikiano wa Tehran na Muscat katika uga wa kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kakdhalika. 

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa, katika ushirikiano wake na majirani, Tehran inaheshimu misingi ya ujirani mwema, kuheshimiano pande mbili na maelewano.

Ali Shamkhani amebainisha kwamba, hatua za baadhi ya nchi katika eneo pamoja na miamala yao ya pupa na ya kijeuri imeondoa anga ya maelewano na mazungumzo na wakati huo huo, kulifanya suala la kukabiliana na migogoro ya eneo kukabiliwa na changamoto kubwa.

Yusuf bin Alawi Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Oman (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Dakta Muhammad Javad Zarif

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameonyesha kusikitishwa kwake na kuendelea hujuma na mashambulio ya kijeshi dhidi ya Yemen na mauaji dhidi ya raia wasio na hatia na kusisitiza kuwa, utatuzi wa mgogoro huo si mtutu wa bunduki.

Kwa upande wake, Yusuf bin Alawi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Oman amesisitiza udharura wa kustafidi na tajiriba ya huko nyuma kwa ajili ya kuzuia kushadidi mizozo na mivutano katika eneo kkatika eneo la Mashariki ya Kati.