-
Meja Hussein Salami: Hakuna ndege yoyote isiyo na rubani ya Iran iliyotunguliwa
Jul 24, 2019 23:18Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) aliyekuwa ametembelea maeneo yaliyokumbwa na mafuriko ya mkoa wa Lorestan, amesema: "Natangaza rasmi kuwa hakuna ndege yoyote isiyo na rubani ya Iran iliyotunguliwa."
-
Rais Rouhani: Iran haitasalimu amri kwa njia ya kuketi kwenye meza ya mazungumzo
Jul 24, 2019 07:10Rais Hassan Rouhani amesisitiza kuwa: Iran iko tayari kikamilifu kufanya mazungumzo ya kiadilifu, kisheria na yenye kulinda izza na heshima yake, lakini haitasalimu amri kwa njia ya kuketi kwenye meza ya mazungumzo.
-
Mshauri wa Amiri Jeshi Mkuu wa Iran atoa onyo kwa Marekani na Uingereza
Jul 24, 2019 13:25Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya ulinzi ametoa onyo kwa Uingereza kuhusiana na nia yake ya kujiingiza kwenye eneo la Lango Bahari la Hormuz na kwa Marekani kuhusu nia yake ya kutaka kuanzisha vita vya kijeshi na akaeleza kwamba: Kauli iliyotolewa na Saudi Arabia na Imarati kuhusu kuhitimishwa vita vya Yemen inadhihirisha kushindwa kwao katika vita hivyo.
-
Iran yapinga matamshi ya kifidhuli na kibaguzi ya Trump kuhusu taifa la Afghanistan
Jul 24, 2019 02:48Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Iran amelaani matamshi ya kibaguzi na kifudhuli yaliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya taifa la Afghanistan.
-
Mazungumzo ya Dakta Zarif nchini Bolivia; kituo cha mwisho cha safari yake ya kiduru Amerika ya Latini
Jul 24, 2019 02:46Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameitembelea Bolivia kikiwa kituo chake cha mwisho cha safari yake katika nchi tatu za Amerika ya Latini.
-
Wanachuo wakusanyika mjini Mashhad kumuunga mkono Sheikh Ibrahim Zakzaky
Jul 23, 2019 23:45Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ferdowsi cha mjini Mashhad kaskazini masharikki wa Iran wamefanya mkusanyiko mkubwa na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.
-
Zarif: Kusimamishwa meli ya mafuta ya Iran ni uharamia na kumefanyika kwa amri ya Marekani
Jul 23, 2019 23:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, kitendo cha kusimamisha na kukamatwa meli kubwa ya mafuta ya Iran katika maji ya karibu na eneo la Jabal Tariq ni uharamia na wizi wa baharini na kimefanyika kwa amri ya Marekani.
-
Ali Shamkhani: Iran itaendelea kuunga mkono muqawama wa Palestina hadi utakapopata ushindi
Jul 23, 2019 08:00Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kuiunga mkono Palestina hadi muqawama utakapopata ushindi mbele ya utawala unaoua watoto wa Israel.
-
Mazungumzo ya Waziri Mkuu wa Iraq mjini Tehran; sisitizo la kulindwa usalama na uthabiti wa Mashariki ya Kati
Jul 23, 2019 06:58Adil Abdul-Mahdi, Waziri Mkuu wa Iraq ambaye adhuhuri ya jana Jumatatu aliwasili hapa mjini Tehran akiuongoza ujumbe wa ngazi za juu wa nchi yake; amesema katika mazungumzo yake na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwamba, kuna haja ya kustawishwa uhusiano wa pande mbili na kutekelezwa makubaliano yote yaliyofikiwa kati ya nchi mbili hizo.
-
Rais Rouhani: Uhusiano wa pande zote kati ya Iran na Iraq unazidi kupanuka na kustawi
Jul 23, 2019 03:10Rais Hassan Rouhani amesema, hatua athirifu zingali zinaendelea kuchukuliwa katika kupanua na kustawisha uhusiano wa pande zote kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Iraq.