-
Ayatullah Kashani: Katu Iran haitasaimu amri mbele ya njama za adui
Jun 07, 2019 08:36Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema katu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitasalimu amri mkabala wa njama za maadui na kusisitiza kwamba taifa hili litaendelea kufungamana na muqawama.
-
Iran yakosoa matamshi ya Rais wa Ufaransa alipokutana na Trump
Jun 07, 2019 02:58Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu matamshi ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alipokutana na mwenzake wa Marekani mjini Paris na kusema matamshi ya Macron hayasaidii katika kulindwa mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Viongozi wa Russia na China wasisitiza kuendelea kuheshimiwa mapatano ya JCPOA, walaani vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran
Jun 06, 2019 22:39Russia na China zikiwa nchi mbili muhimu wanachama wa kundi la 4+1 daima zimekuwa zikisisitiza udharura wa kulindwa mapatano ya kimataifa ya JCPOA na wakati huohuo kupinga vikwazo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Iran.
-
Japan: Tunafanya juhudi kwa ajili ya kupunguza mzozo kati ya Iran na Marekani
Jun 06, 2019 12:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan amesema kuwa nchi yake inafanya juhudi kwa ajili ya kupunguza mzozo kati ya Iran na Marekani.
-
Iran: Wananchi wa Palestina ndio waamuzi wa mwisho wa kadhia ya Palestina
Jun 06, 2019 06:35Msemaji wa Baraza la Kutunga Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, msimamo wa Tehran ni kwamba wananchi wa Palestina ndio wenye haki ya kujiamulia wenyewe mustakbali wa nchi yao.
-
Zarif aikosoa Mossad ya Israel kwa kuituhumu Iran kwa ulipuaji wa meli za mafuta al-Fujairah, UAE
Jun 05, 2019 22:45Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepuuzilia mbali 'taarifa za kiintelijensia' za Shirika la Kijasusi la Utawala wa Kizayuni wa Israel Mossad zinazodai kwamba Iran imehusika na kulipuliwa meli za mafuta katika Bandari ya al-Fujairah huko Umoja wa Falme za Kiarabu, akisisitiza kuwa amewahi kutoa indhari huko nyuma kuhusu kupikwa njama za kutaka kuibua taharuki katika eneo.
-
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu; 'Muqawama (ukakamavu)', siri ya ushindi dhidi ya adui
Jun 05, 2019 22:01Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewaambia viongozi na wananchi wa Iran kutohadaika na ujanja wa kisiasa wa rais wa Marekani.
-
Rouhani: Iran inafanya juhudi za kuimarisha usalama wa Asia Magharibi
Jun 05, 2019 07:12Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inafanya juhudi za kuimarisha usalama katika eneo la Asia Magharibi na haina hamu wala nia yoyote ya kuingia vitani na nchi nyingine.
-
Kiongozi Muadhamu: Muamala wa Karne kamwe hautofikia malengo yake
Jun 05, 2019 03:50Kiingozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu sambamba na kusisitiza kwamba mpango unaoitwa 'Muamala wa Karne' hautofikia malengo yake, amepongeza nchi za Kiarabu na kadhalika makundi ya Palestina yaliyopinga mpango huo.
-
Kiongozi Muadhamu: Nchi za Kiislamu zipambane na adui ghasibu anayetenda jinai Palestina
Jun 05, 2019 07:25Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, nchi za Kiislamu zina wajibu wa kukabiliana na adui ghasibu anayetenda jinai huko Palestina na sio kuzozana zenyewe kwa zenyewe.