Ayatullah Kashani: Katu Iran haitasaimu amri mbele ya njama za adui
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i53976-ayatullah_kashani_katu_iran_haitasaimu_amri_mbele_ya_njama_za_adui
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema katu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitasalimu amri mkabala wa njama za maadui na kusisitiza kwamba taifa hili litaendelea kufungamana na muqawama.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 07, 2019 08:36 UTC
  • Ayatullah Kashani: Katu Iran haitasaimu amri mbele ya njama za adui

Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema katu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitasalimu amri mkabala wa njama za maadui na kusisitiza kwamba taifa hili litaendelea kufungamana na muqawama.

Ayatullah Imami Kashani amesema hayo katika hotuba mbili za Swala ya Ijumaa hii leo hapa Tehran na kuongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu imeionyesha Marekani na waitifaki wake kwamba haiwezi kupigishwa magoti na maadui.

Ameashiria matamshi ya hivi karibuni ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu umuhimu wa umoja na mshikamano miongioni mwa watu, na kusisitiza kuwa wananchi, serikali na vyama mbalimbali vya siasa hapa nchini vinapaswa kufuata nasaha hizo za Ayatullah Ali Khamenei ili wavune matunda halisi ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Ayatullah Kashani amesema Marekani imekuwa ikifanya njama za aina mbalimbali kwa shabaha ya kudhalilisha na kupotosha taswira ya kweli ya Mapinduzi ya Kiislamu tangu yapate ushindi mwaka 1979, lakini sera zake zote hizo zimegonga mwamba.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa hii leo hapa Tehran ameeleza bayana kuwa, “Bila shaka, adui anataka kulipigisha magoti taifa azizi la Iran, lakini wananchi na serikali ya nchi hii wataibuka washindi kutokana na subira yao.”

Ayatullah Imami Kashani

Kadhalika amepongeza mahudhurio makubwa ya wananchi Waislamu ndani na nje ya Iran katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kusisitiza kuwa, maadui wanafanya juu chini kuzusha vita na mifarakano miongoni mwa Waislamu.

Amebainisha kuwa: “Badala ya kupigana wenyewe kwa wenyewe, nchi za Kiislami zinapaswa kuungana na kusimama bega kwa bega dhidi adui ghasibu anayekalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina."

Khatibu wa Swala ya Ijumaa hapa Tehran amesema hakuna chembe ya shaka kuwa Palestina itaibuka mshindi mbele ya utawala wa Kizayuni wa Israel.