Petroli ya Euro 3 yazusha fujo na malalamiko Ujerumani
Kupaa vibaya na kwa kasi bei ya mafuta nchini Ujerumani kumewakasirisha madereva na kuiweka serikali katika mashinikizo ya kutafuta suluhisho la haraka.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim, ongezeko kubwa la bei ya mafuta limewaongezea mzigo madereva nchini Ujerumani na kuilazimisha serikali itafute njia ya kupunguza haraka gharama hizo.
Kwa kawaida vituo vya mafuta nchini Ujerumani vinaruhusiwa kupandisha bei mara moja tu kwa siku — hasa saa sita mchana. Sasa asubuhi ya tarehe 15 Septemba jijini Berlin, bei ya petroli aina ya E10 ilipaa na kufikia takriban Euro 2.25 kwa lita, huku dizeli ikiwa karibu Euro 2.37. Kufikia saa sita mchana siku hiyo hiyo, bei zilipaa tena kwa takriban Euro 0.20 kwa lita na bei ya juu zaidi ilirekodiwa katika kituo cha mafuta cha barabara kuu kusini mwa Berlin, ambapo petroli aina ya "Super Plus" ilifikia Euro 3.03 kwa lita.
Kupaa huko kwa bei kunawaongezea mzigo mkubwa wananchi hasa wa maeneo ya vijijini, kwani — tofauti na miji mikubwa — wakazi wa vijijini nchini Ujerumani hawana njia mbadala za usafiri zaidi ya kutumia gari. Kwa upande mwingine, wakazi wanaoishi karibu na mipaka ya nchi wanaweza kusafiri kwenda nchi jirani kununua mafuta kwa bei nafuu.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Shirikisho la Takwimu la Ujerumani, tarehe 7 Septemba, gharama ya kujaza tangi la lita 60 la petroli aina ya E10 huko Jamhuri ya Czech na Poland ilikuwa rahisi zaidi kwa chini ya Euro 31 kuliko na Ujerumani.
Wakati serikali ya Ujerumani ina wasiwasi mkubwa na unaoongezeka wa kuzidi kupaa bei ya mafuta, Friedrich Merz, mwanasiasa mashuhuri wa Ujerumani, alisema siku ya Jumanne katika hafla iliyoandaliwa na Chama cha Biashara ya Nje cha Ujerumani mjini Berlin kwamba watu wengi wanaotegemea magari yao kila siku wamefika mwisho wa uwezo wao, na hatua lazima zichukuliwe kushughulikia mgogoro huo.
Kabla ya Marekani na Israel kuivamia kijeshi Iran, hali ya nishati haikuwa nzito kiasi hiki duniani.