Iran: Wananchi wa Palestina ndio waamuzi wa mwisho wa kadhia ya Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i53955-iran_wananchi_wa_palestina_ndio_waamuzi_wa_mwisho_wa_kadhia_ya_palestina
Msemaji wa Baraza la Kutunga Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, msimamo wa Tehran ni kwamba wananchi wa Palestina ndio wenye haki ya kujiamulia wenyewe mustakbali wa nchi yao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 06, 2019 06:35 UTC
  • Iran: Wananchi wa Palestina ndio waamuzi wa mwisho wa kadhia ya Palestina

Msemaji wa Baraza la Kutunga Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, msimamo wa Tehran ni kwamba wananchi wa Palestina ndio wenye haki ya kujiamulia wenyewe mustakbali wa nchi yao.

Abbasali Kadkhodaei ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba, mustakbali wa Paelstina unapaswa kuamuliwa na wananchi wenyewe wa Palestina kupitia masanduku ya kura.

Katika ujumbe wake huo, Profesa Kadkhodaei amesema: Msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu kadhia ya Palestina daima ni ule ule wa kimantiki na kidemokrasia na unaochunga misingi yote ya kimataifa, kwamba wananchi wenyewe wa Palestina ndio wenye haki ya kuamua mustakbali wa taifa na nchi yao kupitia masanduku ya kura.

Umati wa wananchi wa Palstina katika maziko ya mmoja wa raia mwenzao aliyeuliwa shahidi kikatili na wanajeshi wa Israel

 

Itakumbukwa kuwa katika hotuba yake aliyoitoa mbele ya umati mkubwa watu kwa mnasaba wa mwaka wa 31 wa kukumbuka siku aliyofariki dunia Imam Khomeini, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alisema, pendekezo la Jamhuri ya Kiislamu ni kuulizwa wananchi wote wa Palestina, Waislamu, Wakristo na Mayahudi pamoja na wakimbizi wa Kipalestina kuhusu mfumo wanaoutaka wa kutawala nchi yao. 

Aidha alisema, mapambano ya kijeshi, kisiasa na kiutamaduni ya Wapaletina lazima yaendelee hadi pale wavamizi na maghasibu wa Kizayuni watakapoheshimu maamuzi ya taifa la Palestina.