-
Qalibaf aonya kuwa Iran italipiza kisasi kwa kushambulia rasilimali za nishati za Marekani
Sep 08, 2026 04:36Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, ametoa onyo kali kwa Marekani kwamba shambulizi lolote dhidi ya rasilimali za mafuta na gesi za Iran litajibiwa kwa hatua sawa, akisisitiza kuwa makampuni na miundombinu ya nishati ya Marekani katika eneo hili iko katika hali sawa ya hatari.
-
Qalibaf aukejeli utabiri wa Waziri wa Hazina wa Marekani kuhusu bei ya mafuta
Sep 07, 2026 11:17Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amepuuzilia mbali utabiri wa Waziri wa Hazina wa Marekani, Scott Bessent, kwamba bei ya mafuta itashuka hadi dola 40 kwa pipa, akiutaja kuwa “ni mawazo na ndoto.”
-
Baghaei: Uhusiano wa Iran na China ni mzuri sana, na mawasiliano yanaendelea katika ngazi mbalimbali
Sep 07, 2026 11:00Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran sambamba na kusisitiza kuendelea uhusiano mzuri na wa kirafiki kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na China amesema, “Mawasiliano kati ya nchi hizo mbili yanaendelea kwa utaratibu na kwa mfululizo katika ngazi mbalimbali, na Iran itatumia fursa zilizopo mbele yake, zikiwemo Mkutano wa BRICS, kuendeleza mashauriano na China pamoja na nchi nyingine rafiki.”
-
Kwa nini Marekani inakanusha vita ilivyoanzisha yenyewe?
Sep 07, 2026 06:07Katikati ya mashambulizi ya kulipizana kisasi kati ya Marekani na Iran, White House inaendelea kukwepa kutumia neno "vita," kuhusu mgogoro uliopo na badala yake kutumia ibara za "operesheni za kijeshi" na "hatua chache"; hata hivyo, hali halisi ya mambo, kuanzia mashambulizi ya makombora na vifo au majeruhi hadi kutumwa katika eneo idadi kubwa ya askari na meli za kivita za Marekani, inaonyesha taswira tofauti kabisa.
-
Meja Jenerali Rezaei: Iran itaainisha 'eneo jipya la marufuku' nje ya Mlango-Bahari wa Hormuz
Sep 07, 2026 03:37Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran (SNSC) amesema, eneo jipya la marufuku nje ya Mlango-Bahari wa Hormuz litatangazwa katika siku zijazo, akionya kwamba chombo chochote kitakachoingia katika eneo hilo bila mashauriano na Tehran kitawekwa kwenye orodha ya vikwazo vya Iran.
-
Iran yavunja rekodi ya uzalishaji wa zao la ngano
Sep 07, 2026 03:00Naibu Waziri wa Jihadi ya Kilimo anayesimamia masuala ya uzalishaji wa mazao nchini Iran ametangaza kuvunjwa rekodi ya uzalishaji wa ngano akisema: “Mwaka huu, kwa mara ya kwanza katika historia, taifa hili limefanikiwa kuzalisha tani milioni 14.1 za ngano nchini, kiwango ambacho kinachukuliwa kuwa kikubwa na cha kuzingatiwa.
-
Qalibaf: Marekani inapaswa kujua kwamba enzi ya "majibu sawia" imekwisha
Sep 06, 2026 11:38Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa kabla ya kuchelewa, Wamarekani wanapasa kujua kwamba kanuni za mchezo zimebadilika na kuanzia sasa, uchokozi wowote dhidi ya maslahi na usalama wa Iran utajibiwa kwa hatua itakayokuwa "ya haraka zaidi, nzito zaidi na yenye kuumiza zaidi."
-
Admeri Sayyari: Uwezo wa Iran wa kuzuia mashambulizi umeongezeka pakubwa/ Taifa la Iran haliwezi kushindwa
Sep 06, 2026 11:36Naibu Mkuu wa Jeshi la Iran amesema kuwa uwezo wa Jamhuri ya Kislamu wa kuzuia mashambulizi dhidi umeimarika pakubwa.
-
Makombora ya Balistiki ya IRGC yalazimisha meli za Kivita za Marekani kutoroka
Sep 06, 2026 04:20Kikosi cha Anga za Juu cha Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimerusha makombora kadhaa ya balistiki kuelekea kwenye manowari mbili za Marekani ikiwemo ile yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita na kuzilazimu kutoroka. Meli hizo za kivita zilikuwa zikishiriki katika mzingiro haramu wa baharini wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Kuanzia Reuters hadi The New York Times: Ushahidi wa Kushambuliwa Sherehe ya Harusi huko Kuhestak kwa Silaha za Marekani
Sep 06, 2026 03:54Kitendo cha kikatili cha Marekani huko Kuhestak, Sirik, kusini mwa Iran, hakiwezi tena kufichwa nyuma ya simulizi kinzani zinazoenezwa kuhusu vita. Vyombo vya habari vya Magharibi, wataalamu, na wanasiasa sasa wanazungumzia hadharani ushahidi unaoonyesha kuwa silaha za Marekani zilitumika kushambulia moja kwa moja sherehe ya harusi, na kusababisha vifo na majeraha kwa raia waliokuwa wakishiriki sherehe hiyo.