-
Makamu wa Rais: Iran imezishinda njama za kijeshi, imejiweka tayari kwa vita vya kiuchumi
Sep 06, 2026 03:01Makamu wa Kwanza wa Rais Mohammad Reza Aref amesema Iran imezishinda njama za mtawalia za kijeshi, kiuchumi, kijamii na kisiasa zilizolenga kuipindua Jamhuri ya Kiislamu au kuifanya isalimu amri, na kwamba sasa inajiandaa kukabiliana na awamu mpya ya vita vya kiuchumi.
-
Mkuu wa Idara ya Mahakama Iran ataka nchi za BRICS kuwashtaki wahalifu wa kivita
Sep 05, 2026 12:06Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran ametaka nchi wanachama wa BRICS kulaani kukiukwa mamlaka ya Iran na kuwasaka wahusika wa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa wakati wa vita vya Marekani na utawala wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Marekani Yakata Tamaa Kimkakati: Kuanzia Kushindwa Kijeshi hadi Vita vya Kiuchumi Dhidi ya Iran
Sep 05, 2026 07:03Katika onyesho jingine la ubabe na upuuzaji wa sheria za kimataifa, Scott Bessent, Waziri wa Fedha wa Marekani amezitishia nchi huru kuhusu ushirikiano wao na Iran, akisema kwamba hakuna mtu yeyote anayepaswa kuiunga mkono Tehran.
-
Jeshi la Iran lililenga ndege 370 za adui katika vita vya Marekani na Israel
Sep 05, 2026 03:16Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Iran kililenga zaidi ya ndege 370 za kivita za adui zikiwemo zenye rubani na zisizikuwa na rubani au droni wakati wa uchokozi wa hivi karibuni wa Marekani na Israel.
-
China na Iran zaahidi kupanua ushirikiano wa kimkakati katika nyanja zote
Sep 05, 2026 03:02Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran, Gholam-Hossein Mohseni Ejei, amesisitiza tena “azma” ya Iran ya kupanua uhusiano na China, akisisitiza kuwa ushirikiano imara wa kisheria na kimahakama unaweza kuwa nguzo ya mahusiano mapana ya kimkakati kati ya nchi hizo mbili.
-
Sayyid Khatami: Vita vya leo dhidi ya Iran ni vita mseto
Sep 04, 2026 10:54Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, hivi sasa Iran inakabiliwa na vita mseto kutoka kwa adui na kwamba hata vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Waislamu vilianza tangu enzi za Mtume Muhammad SAW mwanzoni mwa Uislamu.
-
Iran yaiambia Jordan: Mnataraji tusubiri hadi lini kutomjibu mchokozi?!
Sep 04, 2026 10:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amejibu matamshi ya hivi karibuni ya waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Jorda kwa kumuuliza: Mnataraji Jamhuri ya Kiislamu ya Iran isubiri hadi lini kutomjibu mchokozi ambaye haheshimu haki ya kujitawala nchi za Kiarabu wala haki za Iran?
-
Reuters: Marekani ndiyo iliyoshambulia sherehe ya harusi nchini Iran
Sep 04, 2026 10:44Baada ya kukiri New York Times, sasa ni zamu ya shirika la habari la Reuters kukiri na kuripoti kwamba, lina ushahidi wa wataalamu wanne wa silaha wanaothibitisha kuwa Marekani ndiyo iliyoshambulia moja kwa moja wananchi waliokuwa kwenye sherehe ya harusi huko Sirik kusini mwa Iran.
-
Qatar imethibitisha kuwa mashambulio ya Iran ndani ya ardhi ya nchi hiyo yalilenga vituo vya kijeshi tu vya Marekani
Sep 04, 2026 03:22Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, ameashiria hati rasmi ya Qatar iliyowasilishwa kwa Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) ikithibitisha kwamba operesheni halali za kujihami za Jamhuri ya Kiislamu dhidi ya vikosi vya Marekani vilivyoko katika ardhi ya Qatar zilielekezwa kwenye vituo vya kijeshi tu vya Marekani.
-
Meja Jenerali Vahidi: Damu isiyo na hatia ya mashahidi madhulumu wa Kohestak haitapotea
Sep 04, 2026 03:20Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe maalumu na kusema kuwa: Damu isiyo na hatia ya mashahidi waliouliwa kidhulma na magaidi wa Kimarekani huko Kohestak haitapotea kamwe na wahusika wakiwemo makamanda waliofanya jinai hiyo ya kivita wataburuzwa mahakamani.