Iran: Chanzo cha uungaji mkono wowote kwa jeshi Marekani ni shabaha halali
-
Makao Makuu ya Majeshi ya Iran, Khatamul-Anbiya (SAW)
Makao Makuu ya Majeshi ya Iran, Khatamul-Anbiya (SAW) yametangaza kuwa chanzo chochote cha uungaji mkono unaotolewa kwa "jeshi vamizi la Marekani" katika mashambulizi dhidi ya mamlaka ya kujitawala na ardhi nzima ya Iran ni shabaha halali ya vikosi vya ulinzi.
Taarifa ya leo ya Khatambul- Anibya imeeleza haya kufuatia tangazo la awali kwamba jeshi la Marekani limeshambulia maeneo ya kusini mwa Iran; hatua iliyokiuka makubaliano ya kusitisha na hujumailiyofanywa wakati mwili wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ukiwa nchini Iraq kwa ajili ya kuagwa.
"Vikosi vyetu vya ulinzi vitaoa "jibu kali" dhidi ya uchokozi na vitendo vya kigaidi vya Marekani. Kamwe" havitaruhusu Marekani uwepo au usimamizi wa Marekani katika Lango Bahari la Hormuz," imeeleza taarifa ya Makao Makuu ya Majeshi ya Iran.
Aidha imesisitiza kuwa: Makao Makuu ya Majeshi ya Iran Khatamul- Anbiya imesisitiza kuwa: Njia pekee salama kwa meli za kibiashara na za kubeba mafuta kupita katika njia hiyo muhimu ya majini ni ile iliyotengwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC na jeshi la Iran usiku wa kuamkia leo yamejibu uchokozi wa Marekani kwa kushambulia kambi za kijeshi huko Kuwait na Bahrain baada ya Marekani kushambulia kusini mwa Iran.
Katika jibu la awali dhidi ya uchokozi huu, vikosi vya wanamaji na anga vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kupitia operesheni ya pamoja ya makombora na ndege zisizo na rubani vimefanya mashambulizi dhidi ya maeneo 85 ya vituo muhimu vya kijeshi vya Marekani katika Bandari ya Salman, Kikosi cha Tano cha Wanamaji nchini Bahrain (Kituo Kikuu cha Jeshi Wanamaji la Marekani eneo la Asia Magharibi), na Kituo cha Anga cha Ali al-Salem nchini Kuwait, na kutungua ndege moja ya adui aina ya MQ9 iliyokuwa ikikusudia kuingilia operesheni hiyo."